NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa elimu ya Udhibiti ubora katika Maonesho ya Bidhaa za Ndani yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam ambapo wajasiriamali wameendelea kutembelea banda lao kwaajili ya kupatiwa huduma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 9,2022 kwenye Maonesho hayo Mkaguzi Msaidizi kutoka TBS, Bw.Issa Dadi amesema katika mchakato wa kupata leseni au kusajili bidhaa au majengo ulikwama basi wapo tayari kutatua changamoto hiyo kwenye maonesho hayo.

"Tanatoa huduma mbalimbali ikiwemo wanaotaka kufahamu namna ya kutaka kuthibitisha bidhaa zao, kufahamu utaratibu wa kusajili majengo ya chakula na vipodozi lakini pia kusajili bidhaa za chakula na vipodozi kama utatoa nje ya nchi na kuziingiza nchi utapewa utaratibu". Amesema

Amesema muitikio wa wananchi katika maonesho hayo ni mkubwa, kwani wajasiriamali wengi wametembelea banda la TBS kwaajili ya kupatiwa huduma hasa kutaka kupata utaratibu wa kusajili bidhaa zao.

"Tunatarajia baada ya maonesho haya, kupokea wajasiriamali wengi sana ambao watakwenda kuthibitisha bidhaa zao na huenda wakatusaidia kutimiza majukumu ya Shirika la Viwango kwenda kuwapatia watanzania bidhaa ambazo ni bora". Amesema
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: