OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki amewaelekeza wataalamu wa TARURA Wilaya ya Same kufika kwenye daraja lililokatika la Makanya - Suji kuona ni hatua gani ya haraka inaweza kuchukuliwa ili kurejesha mawasiliano ya eneo hilo.
Waziri Kairuki ametoa agizo hilo wakati akiwasimika Machifu wa Kipare kwenye hafla iliyofanyika kwenye Kata ya Suji wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.
Agizo la Waziri Kairuki limetokana na wananchi kuelezea adha wanayoipata baada ya kuvunjika kwa daraja hilo.
Mwananchi wa Kijiji cha Suji, Gurisha Mchome amesema wakati wa mvua inabidi watembee mpaka Makanya ambapo kuna njia ya kupandisha mpaka kufika Suji tofauti na wakati daraja hilo halijakatika walikua wanatumia muda mfupi kufika Suji.
Daraja la Makanya-Suji lilikatika wakati wa mvua za vuli za mwaka 2021 na kupelekea adha kwa wananchi wa eneo la Suji wanaolazimika kutumia njia ambayo si rafiki msimu wa mvua kutokana na kujaa maji.
Post A Comment: