Na Dotto Mwaibale, Singida
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Singida limetoa pikipiki 10 zenye thamani ya Sh.25 Milioni kwa wilaya zote kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi sambamba na utoaji wa huduma za haraka kwa wananchi.
Mpango huo wa kununua pikipiki hizo ambao umeanzishwa na Tanesco Mkoa wa Singida unakwenda kuondoa changamoto iliyokuwepo ya kuwafikia wananchi wakati wanapokuwa na shida za dharura ambapo walikuwawakichelewa kuzipata kutokana na kukosekana kwa usafiri kwa shirika hilo kuwa na magari machache ambayo yanakuwa maeneo mengine kwa shughuli za kikazi na kusababisha wafanyakazi wa shirika kushindwa kuwafikia kwa haraka.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi pikipiki hizo iliyofanyika Kijiji cha Kamunyanga Kata ya Aghondi wilayani Manyoni Mkurugenzi wa Tanesco Kanda ya Kati, Mhandisi Frank Chambua alisema pikipiki hizo zinakwenda kutoa huduma katika vitongoji au viunga ambavyo vipo mbali na mjini kwa ajili ya kusogeza huduma kwa wananchi.
“Inapotokea tuna gari moja kwa mfano lipo makao makuu ya wilaya na wakati huo huo wananchi zaidi ya kumi wakapiga simu kwapamoja wakihitaji wahudumiwe inakuwa vigumu kwa gari hilo kwenda kwa mtu mmoja mmoja kwa ajili ya kutoa huduma mpaka litakapo mfikia mteja wa mwisho ni hakika atakuwa amechelewa kupata huduma na ndio maana tukaamua kuanzisha utaratibu huu wa kutumia pikipiki mbazo zitakuwa kulekule kwenye viunga” alisema Chambua.
Alisema mteja akipiga simu ya jambo lolote la dharura itapokelewa ofisi za Tanesco za wilaya husika ambapo watatuma meseji kwenda kwa mfanyakazi wa shirika hilo aliyopo eneo alipo mteja na kutoa huduma haraka na kuwa utaratibu huo utakuwa unatoa huduma ndani ya nusu saa mpaka masaa manne tangu mteja apige simu yakuomba kuhudumiwa.
Mhandisi Chambua alisema mara nyingi matukio mengi ya dharura wanayoyatoa wateja hayahitaji kwenda na gari kubwa na ndio maana wameanzisha mpango wa matumizi ya pikipiki ambao ni rahisi kumfikia mteja kawa haraka na maeneo mbalimbali waliopo.
Chambua alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kuwa makini wanaposafisha mashamba yao yaliyopo chini ya nguzoza za umeme kwa kutumia kuchoma moto kwani mara nyingi wamekuwa wakiunguza nguzo na kulisababishia hasara shirika hilo.
Meneja wa Tanesco Mkoa wa Singida, Mhandisi Frolence Mwakasege alisema Serikali imetumia fedha nyingi kununua pikipiki hizo hivyo akaomba wafanyakazi wa shirika hlo watakao kuwa wakizitumia wazitunze na akawaomba wananchi pale watakapoona zikitumika vibaya watoe taarifa kupitia namba ambazo shirika hilo imezitoa.
“Pikipiki hizi ni mali ya serikali na serikali ni mimi na ninyi wananchi ombi langu kwa walewatakao kuwa wakiitumia wanatakiwa kuzitunza na kuzilinda na zitumike kwa kazi iliyokusudiwa” alisema Mhandisi Mwakasege.
Aidha Mwakasege aalisema shirika hilo litakwenda kufunga umeme katika Zahanati ya Kijiji cha Kaminyanga kufuati ombi lililotolewa na Diwani wa Kata ya Aghondi,Emmanuel Sogweda.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Mwagisa aliishukuru Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya mambo makubwa katika sekta ya umeme ambapo katika wilaya hiyo kila sehemu nishati hiyo ya umeme imefika na kuwa katika vijiji 58 katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ni vijiji 20 pekee ndivyo bado havijapata nishati hiyo.
Neema Andrew akiungumza kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo aiipongeza Serikali na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kuwapelekea pikipiki hizo ambazo zinakwenda kuboresha utendaji kazi na kuwafikia wananchi kwa wakati watakapo kuwa wakihitaji huduma mbalimbaliza shirika hilo.
Mkurugenzi wa Kanda ya Kati wa shirika hilo, Mhandisi Frank Chambua, akizungumza kwenye hafla hiyo. |
Meneja wa Tanesco Mkoa wa Singida, Mhandisi Frolence Mwakasege, akizungumza. |
Mwaipopo akizungumzia huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo ikiwepo huduma mpya ya maombi ya kuunganishiwa umeme kwa njia ya mtandao iitwayo NIKONEKT ambayo inafanyika kwa kutumia simu ambapo muombaji anaomba akiwa nyumbani bila ya kufika ofisi za shirika hilo.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikindelea.
Wananchi wakiwa kwenye hafla hiyo.
Pikipiki zikishushwa kwenye gari kwa ajili ya kukabidhiwa.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Aghondi, Nuru Hamisi akizungumza kwenye hafla hiyo alilishukuru Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kutoa pikipiki hizo na hatua walioifikia ya kuweka umeme katika Zahanati ya kijiji hicho kwani utasaidia wananchi hasa wajawazito pia aliishukuru Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kutekeleza miradi mbalimbali kwa kutoa fedha nyingi.
Muonekano wa pikipiki hizo.
Diwani wa Kata ya Aghondi, Emmanuel Sogweda akichangia jambo kwenye hafla hiyo.
Meneja wa Tanesco Wilaya ya Manyoni Mhandisi James Mushi akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kaminyanga katika hafla hiyo.
Post A Comment: