Na Denis Chambi, Tanga. 

KAMATI  ya Usajili ndani ya klabu ya Wagosi wa Kaya Coastal Union imebainisha kuwa iko mbioni kuingia chimbo kusaka baadhi ya wachezaji watakaokuja kukiongezea nguvu kikosi hicho ili kiweze kufanya vizuri kunako ligi kuu ya Tanzania bara NBC msimu huu wa 2022/2023. 

Akizungumza  mwenyekiti wa kamati ya usajili ya wagosi hao Ahmmed Aurora amefunguka kuwa watasajili wachezaji watatu ambao ni pendekezo kutoka kwa mwalimu huku wakiwaacha wengine na kuvunja nao mikataba wale ambao hawajatimiza vigezo na masharti waliyopewa wakati wanatia saini kukitumikia kikosi hicho cha wagosi wa kaya

 "Tumepokea ripoti ya mwalimu na tayari tunayo tunaifanyia kazi kutokana na matakwa yake kuna nafasi za wachezaji watatu kwahiyo ni kweli tutasajili na tayari kuna wachezaji amewapendekeza na tuko kwenye mazungumzo nao"

 "Kuna wachezaji wetu tumewaongezea mikataba mfano kama Majimengi ana mkataba mpya isipokuwa kuna wachezaji wengine tutawapunguza hilo liko wazi wachezaji wengine wamemaliza mikataba yao lakini wengine mwalimu hawahitaji tunakwenda kuvunja nao mkataba tutatumia vipengele ambao tulivitumia wakati wa kusajili ikiwa hawajafikia malengo ya timu" alisema Aurora.

 Mwenyekiti huyo wa kamati ya usajili ameongeza kuwa bado kocha wao mkuu Yusuph Chipo raia wa Kenya yupo sana tu hii ni kutokana na kuridhishwa na mwenendo wa timu tangu alipokabidhiwa kukinoa kikosi hicho kilichokuwa kwenye mikono ya aliyekuwa kocha wao Juma Mgunda aliyetimkia Simba SC.

 "Nafasi ya mwalimu bado ni kubwa sana bado tuko naye kwa sababu licha ya timu kutokufanya vizuri sana , sio yeye alisajili kwahiyo amekuja ni mpya na amekuta wachezaji ni wapya kwake kwahiyo bado nafasi yake ni kubwa kwetu sisi na yupo anatengeneza timu"

 Coastal Union ambao mpaka sasa wameshacheza michezo yao 15 wamejikusanyia poinyi 15 pekee wakiwa nafasi ya 12 kunanko msimamo baada ya kushinda mara 4 vipigo 8 na sare 3 walizozipata mpaka sasa kwenye msimu huu wa ligi ya NBC 2022/2023.




Share To:

Post A Comment: