Na Dotto Mwaibale, Singida.
MBUNGE wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima amedhamini na kuzindua mashindano ya ligi ya mpira wa miguu ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) katika Kata ya Minga yajulikanayo Minga Cup.
Mashindano hayo yaliyozinduliwa jana katika Uwanja wa Shule ya Msingi Minga yamelenga kuwaweka pamoja vijana wa kata hiyo sanjari na kuimarisha afya zao
Kwenye uzinduzi huo Mbunge Sima alitoa mpira kwa ajili ya mashindano hayo ambayo fainali yake inatarajiwa kuwa Desemba 31, 2022.
Akizungumza na washiriki wa mashindano hayo Sima alisema michezo ni afya,ajira,upendo,mshikamano na kuwa inaleta urafiki,umoja,ujamaa,ushirikiano katika masuala mbali mbali.
Aidha Sima aliahidi kuendelea kuwaunga mkono vijana katika jimbo hilo katika masuala mbalimbali yenye tija ikiwemo michezo.
Katika uzinduzi huo Mbunge Mussa Sima aliongozana na Diwani wa Kata ya Mwankoko, Emmanuel Emadaki.
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Minga, Masanja Christopher akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo.
Diwani wa Kata ya Minga, Ibrahim Mrua akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Mbunge wa Singida Mjini Mussa Sima akimkabidhi mpira Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Minga, Masanja Christopher.
Mbunge wa Singida Mjini, Mussa Sima (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji na washiriki wa uzinduzi wa mashindano hayo.
Post A Comment: