Na,Jusline Marco;Arusha
Taasisi Atamizi ya DTBi- COSTECH ya jijini Dar es salaam imeshindanisha shule 7 za Mkoa wa Arusha katika ubunifu ili kutatua changamoto katika jamii kupitia miradi inayofanywa na taasisi ya Future STEM Business Leaders kwa kushirikiana na Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) na chuo kikuu Dar es salaam.
Akizungumza jijini Arusha katika mashindano hauo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Taasisi hiyo Dkt. Erasto Mlyuka ameitaka jamii kuendeleza misingi ya vijana kuja na suluhu ya changamoto zilizopo katika nchi kwa kubadilisha thamani ya elimu kuwa zao na huduma.
Dkt .Mlyuka alisema kuwa mradi huo umetokana baada ya mapitio ya taasisi ya fizikia ya uingereza kuona changamoto katika Dunia kuwa wanafunzi wengi kuyopenda masomo ya sayansi na kukimbilia kwenye masuala ya biashara huku jamii ikishindwai kufanya biashara bila kuwa na vitu vinavyotokana na masomo ya kisayansi.
Aidha ameeleza kuwa kwa sasa wapo kwenye hatua ya kuhakikisha mfumo wa programu hiyo unaohusisha Mwalimu, Mwanafunzi na wataalamu wa biashara ambao wapo sokoni unaendelezwa nchi nzima.
“Niwapongeze wanafunzi wote, mmeanza safari ya ubunifu, hamtakaa mlale, ubunifu unahitaji kujitoa, kujali wengine na kujituma kwahiyo naamini zawadi mlizozipata na vyeti mlivyotunukiwa vitawakumbusha na kuwafanya mjione kumbe mnaweza,” Alisema.
Awali Mkuu wa chuo cha ufundi Arusha (ATC) Dkt. Musa Chacha akizungumza alisema kuwa ni vyema kwa mradi huo kuona fizikia kama fursa kwa wanafunzi kwani tatizo kubwa ni maarifa ambayo wanapatiwa watoto.
Naye Kaimu Mkuu wa chuo cha ATC Dkt .Yusuph Mhando alisema taifa lina tatizo la ajira kwa vijana na suluhisho ni bunifu za kisayansi zilizofanyika katika mashindano hayo ambapo zikiendelezwa zitatoa suluhu ya changamoto zilizopo kwenye jamii pamoja na kutoa ajira kwa vijana
Kwa upande wake Meneja wa mradi wa Future STEM Business Leaders Josephine Sepeku alisema kuwa mradi huo unalenga kujenga na kutatua changamoto za biashara pamoja na sayansi kwa kuwafundisha wanafunzi wanaosoma ya sayansi kutumia sayansi za darasani kuzileta katika mfumo wa biashara.
“Tunaposema vijana wajiajiri, tunaposena Tanzania ya viwanda tunaanzia hapa, tunawapatia mafunzo ili wao waweze kutengeneza na Leo tumekuwa na shule saba ambazo zimeweza kushiriki, wanafunzi wakiwa ni 35 na wameweza kuja na bunifu mbalimbali na tumeweza kupata washindi watu,” Alieleza.
Sambamba na hayo matokeo ya mashindano hayo yalitaja mshindi wa kwanza kuwa ni shule ya Arusha girls ambao wamekuja na kifaa cha utunzaji wa mazingira,kinachotunza usafi wa mazingira lakini pia kuleta biashara baada ya mkaa unaotoka katika kifaa hicho baada ya taka kuwekwa unaweza kutengenezewa matofali.
Vilevile mshindi wa pili katika mashindano hayo ameweza kuleta suluhu ya changamoto zinazokumba jamii kwa kuja na mfumo unaoweza kupunguza ajali zinazotokea kutokana na kutokuelewa maeneo ya barabara au kutokufuata sheria pamoja na mshindi wa tatu ambaye ameweza kutengeneza mbolea isiyo na kemikali.
Post A Comment: