Mashindano ya mpira wa wavu maarufu kama MAVUNDE CUP yamezinduliwa rasmi leo katika shule ya Msingi Mlezi Jijini Dodoma huku yakijumuisha Timu 18 za wanaume na wanawake kutoka mkoani Dodoma na nje ya Dodoma.


Mashindano hayo yamezinduliwa leo na Diwani wa Kata ya Hazina Mh. Samwel Mziba akiongozana na Diwani wa Viti Maalum Mh. Flora Lyacho huku wote wakitoa rai kwa Vijana wa Dodoma kuchukua fursa ya haya mashindano kama sehemu ya kuendeleza na kukuza vipaji vyao.



Zoezi hili la uzinduzi wa mashindano limekwenda sambamba na ugawaji wa vifaa vya michezo kwa Timu zote zinazoshiriki katika mashindano hayo pamoja na ukarabati wa kiwanja cha kuchezea.

Mashindano hayo yatafikia tamati siku ya Jumapili,ambapo Mgeni Rasmi wa mashindano hayo anatarajiwa kuwa Anthony Mavunde Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Mfadhili wa mashindano hayo.

Share To:

Post A Comment: