Mdhamini wa ligi ya machupa Super Cup Thoma Daffa (kulia) akikabidhi kombe la ubingwa kwa nahodha wa timu ya Majengo United Shabi Tupa mara baada ya kutwaa taji hilo mbele ya timu ya Tallent kwa mikwaju ya penati 4-2 jumaanne hii kwenye uwanja wa Magomeni jijini Tanga.
Timu ya Majengo United imetawadhwa kuwa mabingwa wa Machupa Super Cup kwa ushindi wa mikwaju ya penati 4-2 walioupata mbele ya Vijana wa Tallent FC walipokutana kwenye fainali ya kuamua nani bingwa atakayeondoka na zawadi ya Ng'ombe, Kombe na jezi katika michuqno hiyo iliyofanyika ndanibya kata ya Duga jijini Tanga.
Fainali hiyo iliyopigwa juzi jumanne katika uwanja wa Magomeni jijini hapa unaweza kusema ilikuwa ni bahati yao Majengo United baada ya kuchomoa goli dakika ya 89 ya mchezo walilokuwa wametanguliwa na wapinzani wao mapema kabisa mwa kipindi cha pili hivyo ufundi wa kupiga mikwaju ya penati ukawakosesha Tallent ubingwa huo.
Licha ya timu ya Tallent kupoteza ubingwa wa michuano hiyo lakini wamejikusanyia zawadi nyingi zaidi ukiachana na zile za mshindi wa pili ambazo ni jezi seti moja na mipira mitano , wakiongoza kwenye timu yenye nidhamu, Kipa bora Haruna Ally , Kocha Bora Seleman Hamis Mchezaji bora Sadick Abubakary wote hao wametokea timu yao huku kipa bora Ruga Ally akitokea kwa mabingwa Majengo United na Said Danga akitangazwa kuwa ndiye muamuzi bora wa mashindano hayo.
Akizungumza mara baada ya michuano hayo mdhamini wa ligi Thomas Daffa alisema kuwa baada ya kupata wazo la kuanzisha ligi za ndondo aliangalia ni wapi waandaaji wengi wanakwama ili naye aboreshe na alifanikiwa kwa namna yake akiwavuta na kuwashawishi wana michezo wadau na wapenzi wa soka jijini Tanga ambao anaamini watakuwa wamejifunza kitu cha utofauti kutoka kwake kupitia ligi hiyo hukua akiahidi kwa mwaka 2023 kuja kivingine zaidi ya hapo.
"Siku zote ukitaka kuboresha ni lazima kuangalia mapungufu ya wengine , wameanzisha ligi wengi nmeangalia kipi ambacho wao hawafanyi mimi nifanye lakini pia nilitaka kuheshimisha michezo ya ndondo ambayo imeonekana kama michezo ya kihuni lakini nimeweka mashindano haya yakiwa na tuzo mbalimbali inawezekana ni ndondo Cup ya kwanza ndani ya jiji la Tanga kuwa na aina hii ya tuzo nyingi zaidi na mwakani Mungu akitujalia uzima ninakuja kuboresha zaidi ya hapa" alisema Daffa.
Awali akizungumza afisa michezo wa halmashauri ya jiji la Tanga Michael Njaule alimpongeza muandaaji na mdhamini mkuu wa logi hiyo Thomas Daffa kwa namna ambavyo michuano hiyo iliteka hisia za wapenda soka kutoka viunga mbalimbali wa jiji hilo akiwataka wadau kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanyika katika sekta ya michezo ili kuinua vipaji vilivyopo kwa vijana na hatimaye kuweza kuonekana.
"Tunamshukuru na kumpongeza sana ndugu yetu Machupa kwa kuja na wazo la michuano hii wenyewe tumeshuhudia jinsi gani ligi ilivyokuwa ni ukweli usiopingika kuwa vijana wamecheza mpira safi na vipaji tumeviona ni jambo la mfano na kuigwa na wadau, wapenzi soka ili kuweza kuinua michezo na kutangaza vipaji viweze kuonekana" alisema Njaule.
Fainali hizo ambazo ni kwa mara ya kwanza kufanyika ndani ya jiji la Tanga zilipambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa mziki wa singeli pamoja bongo fleva Seif Shaaban alamaarufu kwa jina la Matonya ambaye alivuta hisia na wananchi kuja kushuhudia boli safi ikitembezwa na vijana waliojaaliwa vipaji na ufundi mwingi miguuni.
Mashabiki na wachezaji wa timu ya Majengo United wakisherehekea ubingwa wa Machupa Super Cup walioupata mbele ya Timu ya Tallent katika uwanja wa Magomeni jijini Tanga.
Kikosi cha timu ya Tallent wakiwa wanafwatilia kinachoendelea uwanjani Magomeni mara baada kukosa kombe la michuanoMachupa Super Cup wakifungwa kwa mikwaju ya penati 4-2 na timu ya Majengo United juzi jumaanne.
Post A Comment: