OR-TAMISEMI


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdini Babu amesema ujenzi wa madarasa ya 125 kwa ajili ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza 2023 yamekamilika na wanafunzi wote wataanza shule kwa awamu moja.


Babu ameyasema hayo leo katika hafla ya kuwaapisha Machifu wa Kipare iliyofanyika katika Kata ya Suji wilayani Same.


Amesema hakuna mwanafunzi atayechelewa kuanza masomo kwa uhaba wa madarasa baada ya ujenzi wa madarasa hayo kukamilika.


Babu amesema Mkoa wa Kilimanjaro ulipokea Sh bilioni 2.5 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 125 na mpaka sasa ujenzi wa madaras hayo umekamilika tayari kwa kupokea wanafunzi.


“Katika mkoa huu jumla ya wanafunzi 33,469 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2023."


Babu ametumia fursa hiyo kumshukuru  Rais Samia kwa namna anavyoendelea kutoa fedha za miradi ya maendeleo kwa sababu mpaka sasa  Wilaya  zote za Mkoa wa Kilimanjaro zimepokea fedha za ujenzi wa hospitali za Wilaya.


Katika hafla hiyo, Chifu Reubern Amani Mnyuku amesimikwa kuwa chifu mkuu wa Wapare.

Share To:

Post A Comment: