Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Kenani Kihongosi amewataka vijana kumsemea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi anayoifanya ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Amesema Rais Dkt Samia ametekeleza miradi mingi ya maendeleo ukiwemo wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ambalo lilianza kujazwa maji jana.
Hata hivyo, amesema vijana hawajitokezi kumsemea Rais Dkt Samia kwa kazi kubwa anayoifanya, jambo ambalo linawapa nafasi wapinzani kupotosha wananchi.
"Serikali imetekeleza miradi mingi sana, wa kusema ni sisi wanaCCM, vijana twendeni tukaseme.
"Tusikubali wapinzani waende wakapotoshe huko na sisi tupo. Twende tukamtetee Rais wetu, imefika wakati anajitetea mwenyewe, vijana tukamsaidie Rais wetu," amesema Kihongosi.
Wakati huohuo, amesisitiza kwamba uchaguzi katika jumuiya hiyo umekwisha, hivyo amewataka vijana kuungana pamoja kwenda kufanya kazi.
"Uchaguzi umekwisha, kilichobaki ni kuijenga jumuiya na chama chetu, twendeni tukafanye kazi.
"Kwa sasa hakuna timu ya mtu. Mlioshinda mkafanye kazi, ambao kura hazikutosha pia mkafanye kazi, hiki chama hakimtupi mtu anayekitumikia kweli kweli," amesema
Post A Comment: