Angela Msimbira ARUSHA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki ametaja vigezo kadhaa vilivyozingatiwa katika uchaguzi na upangaji shule za sekondari za serikali kwa wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza mwaka, 2023.
Kairuki ametoa kauli hiyo leo tarehe 14 Disemba, 2022 jijini Arusha alipokuwa akitoa taarifa kuhusu wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023.
Amesema uchaguzi huo umezingatia kigezo cha ufaulu wa mtahiniwa anayechaguliwa na kila mtahiniwa aliyefanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka, 2022 ambaye amepata alama za ufaulu kati ya 121 hadi 300 amechaguliwa na kupangiwa shule ya sekondari ya Serikali.
“ Kwa upande wa shule za bweni, shule zimegawanywa katika makundi matatu ambayo ni sekondari za bweni za wanafunzi wenye ufaulu wa juu zaidi, shule za sekondari za bweni, ufundi na shule za sekondari za bweni Kawaida
Kuhusu shule za sekondari za bweni ufundi, Waziri Kairuki amesema mgawanyo umefanyika kwa kila Mkoa kwa kutumia Kanuni ya kugawa nafasi hizo Kitaifa huku shule 22 za bweni za kawaida zimegawanywa kwa kila Halmashauri kwa kufuata idadi ya watahiniwa hao kwenye Halmashauri za Wilaya na wanaotoka katika mazingira magumu .
“Katika kundi hilo, Wanafunzi kutoka Halmashauri za Majiji, Manispaa na Miji hawakuhusishwa isipokuwa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum
“Kwa msingi huo, sio kila mwanafunzi anayefaulu kwa wastani wa A anaweza kuchaguliwa shule ya bweni. Nimeona nisisitize hili ili kupata uelewa wa pamoja hususani kwa wazazi/walezi na wanafunzi ambao hudhani kwamba mwanafunzi kupata wastani wa A ndicho kigezo pekee cha kuchaguliwa kujiunga na shule za Bweni,”amesema Waziri Kairuki
Aidha, amesema kutokana na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufanya maandalizi mapema ili kuhakikisha wanafunzi wote watakaofaulu Mtihani wa kumaliza Darasa la Saba mwaka, 2022 wanajiunga na elimu ya sekondari ifikapo Januari,
Post A Comment: