Na Mario Mgimba
Njombe
Jamii Mkoani Njombe imetakiwa kutumia michezo kujenga afya , kuimarisha vipaji kwa vijana na kuitumia katika fursa mbalimbali zinazojitokeza.
Yamesemwa hayo na Mkuu wa Mashtaka Mkoa wa Iringa Basilius Nyangachi ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika fainali za mabingwa wa Mpete Diwani Cup 2022 ambapo ameweka bayana namna michezo inavojenga mwili huku akiwataka vijana kutumia michezokatika fursa mbalimbali zinazojitokea
Naye Erasto Mpete Mwandaaji wa mashindano hayo ambaye Diwani wa Kata ya Utalingolo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe aliwaasa vijana kutumia michezo kama fursa huku akiwaomba vijana kuchangamkia mikopo isiyokuwa na riba ya vikundi ambayo inatolewa na Halamashauri ya Mji Njombe kwa vijana ,walemavu na Wanawake ambapo itasaidia kupunguza changamoto za ajira .
“Halmashauri yetu ya mji ina mikopo ya vikundi lakini changamoto inayoonekana vikundi vya vijana hatuchangamkii hiyo fursa,kwa hiyo kupitia haya mashindano ninahamasisha vijana muweze kujiunga kwenye vikundi ili muweze kupata fursa hii ya mikopo isiyokuwa na riba”Erasto Mpete M/Kiti halmashauri ya mji wa Njombe kwenye fainali ya Mpete Diwani Cup.
Tumain Mtewa Diwani wa Viti maalumu kata ya Njombe mjini alisema vijana wawenachachu ya kucheza mashindano makubwa na vilabu ambavyo vinacheza mashindano makuwa Afrika ili waweze kuonesha vipaji vyao vitavyo lisaidia taifa.
Chama Myamba mchezaji wa Mfereke FC na Ibrahimu Mligo mchezaji wa Nole FC wameyashukuru mashindano hayo yalivoweza kuibua fursa mbalimbali katika kata hiyo huku wakiahidi kuleta ushindani katika mashindano yatakayo anza mwaka 2023
Baada ya Fainali hiyo Mgeni rasmi alikabidhi zawadi kwa Mfereke FC kwa kuibuka mabingwa kwa Ushindi wa Goli 1-0 ambao walijinyakulia kitita Cha Shilingi 500000/= na Kombe Huku mshindi wa pili ambaye ni Nole FC akibeba kitita cha 300000/= huku mshinda wa tatu Ihalula akibena Shilingi 200000/=
Post A Comment: