Waziri wa nchi, ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa uuma na utawala bora Mhe. Jenister Mhagama amesema miongoni mwa wilaya zinazofanya vizuri katika kushughulikia kero za watumishi wa umma na kutoa huduma bora kwa wananchi Ikungi imeendelea kufanya vizuri zaidi katika ambapo amewapongeza viongozi wa wilaya kwa umoja na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao
Akizungumza wakati wa mkutano wake na watumishi wa umma katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Mhe. Mhagama amesema mpaka sasa tayari madai ya kupandishwa vyeo na madaraja watumishi yameshashughulikiwa kwa asilimia zaidi ya tisini uku wilaya ikiendelea kuboresha mfumo wa utoaji wa huduma bora kwa wananchi
Kutokana na sababu hiyo Waziri Mhagama amewaagiza viongozi wengine Tanzania kwenda kujifunza mfumo bora Ikungi wa kushughulikia masuala ya kero za watumishi na wananchi yanavyotatuliwa
Awali akimkaribisha Waziri Mhagama, Mkuu wa mkoa wa singida Mhe. Peter serukamba amesema katika mkoa wa singida wilaya ya ikungi inaendelea kufanya vizuri katika maeneo yote ya kazi ikiwemo usimamizi wa miradi, masuala ya utumishi wa umma, kushughulikia kero za wananchi pamoja na kusimamia mapato ya serikali na kusisitiza mafanikio hayo yametokana na utendaji kazi wa pamoja baina ya viongozi wa wilaya ya Ikungi
Akitoa taarifa ya wilaya, mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry Muro amesema fedha zote za miradi, na maelekezo ya viongozi wa juu yanayotolewa yametekelezwa kwa asilimia mia moja na haswa katika eneo la usimamizi wa miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma bora kwa wananchi ambapo amemshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa fedha za ujenzi wa hospitali ya wilaya, fedha za ujenzi wa chuo cha veta, fedha za ujenzi wa vituo vya afya vipya 4 na zahanati pamoja ukamilishaji wa upelekaji wa umeme vijijini na katika miradi ya maji na kusisitiza miradi yote inaendelea kutekelezwa vizuri uku mingi ikiwa imeshakamilika kwa ubora
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya za walengwa wa Tasaf awamu ya tatu, Mkurugenzi wa halmashauri ya Ikungi Justice kijazi amesema mpaka sasa tayari kaya 12,268 sawa na asilimia 46 zimeshafikiwa na mpango wa Tasaf uku serikali ikitumia zaidi ya shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya kuzisaidia kaya hizo ambazo baadhi tayari zimeshaanza kubadilisha maisha yao kupitia miradi ya ufugaji na kilimo pamoja na biashara
Waziri Mhagama pia alipata nafasi ya kufanya ziara ya kutembelea kaya wanafaika katika kata ya Mang'onyi kijiji cha Mwau ambapo alizungumza na wananchi na wanufaika hao na kuwakikisha katika mpango ujao atahakikisha wilaya inapewa fedha za miradi ambayo itawahusisha wananchi wenyewe waweze kujiongezea kipato
Post A Comment: