Mwenyekiti wetu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza Tsh Milioni 960 zilizopangwa kutumika kwenye maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru, zikajenge mabweni katika shule 8 za msingi za wanafunzi wenye mahitaji maalum, na badala yake Maadhimisho yatafanyika kwa kufanya shughuli za kijamii na midahalo ngazi za mkoa na Wilaya.
Sisi Jumuiya ya Wanawake wa Tanzania wa Chama cha Mapinduzi CCM (UWT) kwa hakika tunakupongeza Dkt Samia kwa maamuzi haya ya kuhamishia Milioni 960 za Sherehe za Uhuru kujenga mabweni kwani yatakuwa mwarobaini dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa watoto hususani wa kike ambao hutumia umbali mrefu kufika shuleni.
UWT katika kuenzi juhudi zako hizi za kupambana dhidi ya ukatili na unyanyasaji wa watoto, na kwa kutekeleza Ilani ya Chama chetu cha Mapinduzi ya mwaka 2020/2025 Sura ya 6 (117) inayohimiza Serikali kuhakikisha watoto wenu wanapata Elimu bora katika mazingira salama, hivyo tutaanzisha kampeni Nchi zima kupinga aina zote za ukatili dhidi ya watoto.
Jumuiya yetu itaendelea kutoa kila aina ya ushirikiano kwa Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi CCM ili kuhakikisha watoto wetu wote nchini wanapata Elimu bora, wanaepuka changamoto zinazopelekea kufikwa na ukatili wa kijinsia wakati wanatafuta Elimu, na hivyo kama Taifa tutakuwa tumekomesha kesi za ubakaji na aina zingine za ukatili kwa watoto ambazo kwa sasa zinaonekana kuripotiwa kushamiri kwenye Jamii yetu.
MCC Mary Pius Chatanda,
Mwenyekiti wa UWT Taifa.
Desemba 05, 2022.
Post A Comment: