Mkuu wa wilaya Ikungi Mkoani Singida Jerry C. Muro amezindua rasmi mafunzo ya kambi la vijana wa kanisa la waadventista wasabato kwa mkoa wa singida mafunzo yanayofanyika katika kijiji cha mahambe Ikungi
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Dc Muro amewataka wakufunzi kujikita zaidi katika kuwawezesha vijana stadi za maisha zitakazowasadia pia kuepukana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto ma vijana
Dc Muro pia amewataka vijana kushika na kulinda imani zao kama msingi mkuu wa mafanikio na maendeleo yao ya kiroho na maisha na haswa katika kipindi cha ujana ambao umekuwa na changamoto nyingi kwa vijana
Kongamano hilo limewaleta pamoja vijana 170 pamoja na viongozi 15 na wachungaji 5 kutoka katika sharika mbalimbali za kanisa la waadventista wasabato mkoa wa singida Jimbo la Rift Valley.
Post A Comment: