Mdhamini wa ligi ya Machupa Cup Thomas Daffa akimkabidhi Ti-shirt Pamoja na fedha Dolla 10 kipa wa timu ya Tallent Haruna Amiri baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mchezo wa nusu fainali kati ya Tallent dhidi ya Jiwe FC uliochezwa jumapili iliyopita kwenye uwanja wa Magomeni jijini Tanga.
Denis Chambi, Tanga.
Leo jumaane katika dimba la Magomeni jijini Tanga kitaeleweka ni nani bingwa wa machupa Super Cup kati ya Majengo United dhidi ya vijana wa Tallent FC baada ya timu hizo mbili kufanikiwa kutinga hatua ya fainali huku tambo za mashabiki zikizidi kila kona wakitambiana kuwa lazima wqondoke na watwae zawadi zilizoandaliwa.
Kila timu imekiri upinzani waliokutana nao kuwa sio wa kitoto katika hatua ya nusu fainali ambapo Majengo United waliingia fainali baada ya kuitandika Uruguay bao 1-0 wakati Tallent wao wakisonga mbele kwa mikwaju ya penati 4-3 dhidi ya Jiwe FC baada ya kumaliza dakika 90 za mchezo kwa kufungana bao 1-1.
Mdhamini wa ligi hiyo Thomas Daffa amezidi kuboresha katika upande wa zawadi hali ambayo inazidi kuongeza hamasa kwa timu zitakazocheza mchezo huo ambapo bingwa anatarajia kuondoka na Ng'ombe, kombe, jezi seti tano pamoja na mpira mmoja mitano wakati mshindi wa pili yeye akiondoka na mipira mipira mitano.
Juzi jumapili kwenye nusu fainali ya pili ilishuhudiwa goli kipa wa timu ya Tallent FC Haruna Amiri akiondoka na Dolla 10 pamoja na jezi yake baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa hatua hiyo, na sikubya fainali zawadi nyingine zitakwenda kwa Kipa bora, mchezaji bora, mfungaji bora , kiungo bora , kocha bora pamoja na timu yenye nidhamu.
Mdhamini wa ligi hiyo Thomas Daffa alisema kuwa michuano imekuwa na tija kubwa sana kwa upande wa wachezaji waliofanya vizuri kitu ambacho yeye binafsi hakukitegemea kwani baadhi ya wadau wa soka wamekuwa wakitupia jicho kuangalia vipaji kutoka kwa vijana na tayari kuna ambao wameshawishika na wachezaji watatu wakiwa wanawindwa na viongozi wa baadhi ya timu zilizopo jijiini hapa.
"Tunakwenda kwenye fainali na asilimia 95 malengo yametimia ninashukuru Mungu kwa hatua hii tuliyofikia tangu tunaanza mashindano, kuna watu wamekuwa wanafwatilia michuano hiyo nikiri wazi kuwa nmekuwa nikipokea simu za watu mbalimbali , kuna wachezaji kama watatu wameonekana baadaye tutakuja kuwaambia kama mambo yakikaa vizuri na wanafwatiliwa kweli hii ndio ilikuwa plani yangu" alisema Machupa.
Alisema licha ya kwamba ni mara ya kwanza kuanzisha ligi hiyo kuna kitu cha pekee amejifunza kwa msimu ujao akitarajia kujipanga kwa kuwachukua wachezaji ambao wanashirki ligi ya wilaya ili lengo na dhima ya mashindano hayo yaweze kutimia ambayo ni kuinua viwango vya wachezaji wadogo na kuwapa motisha ya kupenda michezo ambapo baadaye wanaweza kuonekana.
"Nimejifunza kwa msimu unaokuja nitaboresha kwenye suala la umri, kwanz nitaenda kuchukua usajili ambao wanasajili ligi ya wilaya zile kadi zao wanazotumia kwenye ligi ya wilaya ndio nitazitumia ili wachezaji hii itasaidia kuwaondoa wachezaji wenye umri mkubwa" alisema
Post A Comment: