DENIS CHAMBI, TANGA.

Naibu waziri wa michezo Paulina Gekul amebainisha kuwa wizara ya  utamaduni Sanaa na michezo ipo mbioni kuanzisha mashindano ya mtaa kwa mtaa yatakayohusisha vijana mbalimbali lengo kuu hasa likiwa ni kuibua vipaji vya Wana michezo watakao unda timu za taifa ambazo zitakuwa zikiiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa.

Akizungumza juzi jumatano kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani katika  uzinduzi wa mashindano ya SHIMIWI' yanayoendelea mkoani Tanga Gekur alisema kuwa Sasa hivi wapo kwenye hatua za mwisho kuhakikisha wanaweka mazingira rafiki ya kufikia adhima hiyo ambapo ni pamoja na kusambaza vifaa vya michezo kote nchini

"Raisi wetu ametuelekeza kuwa hatupaswi kushiriki tu michezo bali tuhakikishe  tunaleta ushindani,  wizara ipo kazini na tunaendelea tunakuja na mashindano ya  mtaa kwa mtaa, tuko katika hatua za mwisho kuhakikisha vifaa vya michezo vinapatikana  ili kule kwenye ngazi za chini tuende kuibua michezo na vipaji mbalimbali  natutakapokuja kwenye ngazi ya taifa tuwe na vijana ambao wamepikwa na kupatikana katika michakato ambayo imefuata taratibu za michezo" 

Alisema mpango wa maendeleo wa taifa  wa miaka 2020/2021 -2025/2026 umebainisha umuhimu wa kuendeleza michezo mbalimbali hapa nchini  pamoja na kutafuta wataalamu na wadau watakaowezesha mpango huo kufanikiwa na kuleta tija kwa sekta ya michezo na Wanamichezo wenyewe.

"Mpango wa maendeleo wa taifa kwa miaka mitano umebainisha umuhimu wa kuendeleza michezo nchini rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akituelekeza na Wizara yetu imekuwa ikitenga fedha na kuhamasisha  kuhakikisha miundombinu inajengwa ili Wanamichezo waweze kushiriki kote nchini"

"Lakini pia suala la wataalamu na kupanua wigo wa  vyanzo endelevu za kugharamia shughuli za michezo , michezo hii ni sehemu ya utekelezaji wa mpango na maendeleo endelevu na ya  umoja wa mataifa michezo ni ajira kubwa duniani nasi lazima tuhakikishe kuwa vijana wetu  wanakuwa katika kupata ajira hiyo.

Share To:

Post A Comment: