Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu (katikati), akibonyesha kitufe kuashiria uzinduzi wa miradi miwili ya Mpango wa Malaria wa Rais wa Marekani (PMI) inayoitwa 'Dhibiti Malaria' unaosimaniwa na Shirika la PSI na 'Shinda Malaria' wa Taasisi ya Afya Ifakara (IHI) yenye thamani ya shs bilioni 103.5 katika hafla iliyofanyika mjini Dodoma hivi karibuni. Kushoto ni Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Donald Wright na kulia Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP), Dk. Samwel Lazaro.



Ni shangwe baada ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu (katikati), kuzindua rasmi miradi miwili ya Mpango wa Malaria wa Rais wa Marekani (PMI) inayoitwa 'Dhibiti Malaria' unaosimaniwa na Shirika la PSI na 'Shinda Malaria' wa Taasisi ya Afya Ifakara (IHI) mjini Dodoma.



Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akizungumza katika hafla hiyo kabla hajazindua rasmi miradi hiyo.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu (kulia), akiwa na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Donald Wright (kushoto), wakati wakaingia katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Serena, Dodoma hivi karibuni, katika hafla ya ufungaji na uzinduzi wa miradi miwili mipya ya Mpango wa Malaria wa Rais wa Marekani (PMI) inayoitwa Dhibiti Malaria unaosimaniwa na Shirika la PSI na Shinda Malaria wa Taasisi ya Afya Ifakara (IHI) yenye thamani ya shs bilioni 103.5.


Balozi wa Marekani nchini, Donald Wright, akizungumza katika hafla hiyo.


Baadhi ya washiriki waliohudhuria hafla hiyo mjini Dodoma hivi karibuni wakifuatilia matukio ya uzinduzi wa Miradi ya malaria inayofadhiliwa na Mpango wa Malaria wa Rais wa Marekani (PMI).



Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu (wa tano kushoto), Balozi wa Marekani nchini, Donald Wright (wa nne kushoto), wakipozi kwa picha ya kumbukumbu pamoja na viongozi wengine.



Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Donald Wright wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau muhimu katika miradi hiyo.

 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Donald Wright wakiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi pamoja na wadau wengine waliowezesha hafla ya uzinduzi huo mjini Dodoma hivi karibuni.
Share To:

Post A Comment: