Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP)Lilian Liundi akitoa elimu katika moja ya Warsha zao nchini Tanzania juu ya kupinga vitendo vya Kikatili kwa Wanawake na Watoto. |
Na John Walter-Manyara
Wazazi na walezi wanaowafanyia ukatili watoto wao kwa kigezo cha adhabu wametakiwa kuacha tabia hiyo kwa kuwa wanawasababishia Usugu katika maisha yao na kupelekea vifo na kukatisha ndoto zao.
Aidha wameshauriwa kutenga muda wa kuzungumza na watoto wao kwa kuwafundisha maadili mema huku wakiaswa pindi wanapotoa adhabu iwe ya kumfunza kitabia na sio kumfanyia ukatili.
Kwenye jamii ya Kitanzania maswala ya haki za mama na mtoto yamekuwa na changamoto kwani wanawake na watoto wako kwenye hatari zaidi kuliko makundi mengine hivyo ni muhimu elimu inayohusu sheria zinazolinda haki zao zifahamike na kuzingatiwa.
Hayo yamesemwa na Wakili Winifrida Manyanga ambae ni mkurugenzi wa Inherital right wakati akizungumza kwenye kipindi cha TOBONGE kinachorushwa Smile Fm redio na kuongeza kuwa kutofahamu sheria kunasababisha watu kushindwa changamoto ya kushindwa kutetea haki zao.
Kwa upande wake mtaalam wa maswala ya saikolojia Anti Sadaka amesema wazazi wanapotoa adhabu hawatoi kwa nia ya kuumiza bali wanatoa adhabu kwa nia ya mtoto aangalie alichokifanya asije kurudia tena.
"Hivyo sifa ya kwanza ya mzazi au mlezi ni kuwa na ule uwezo wa kudhibiti hisia zake anapokuwa na hasira"
Serikali ya Tanzania ikishirikiana na mashirika mbalimbali inazidi kutoa elimu kwa jamii kila uchwao kuhakikisha vitendo vya Ukatili kwa wanawake na watoto vinakomesha huku kukiwa na namba maalum ya kuripoti vitendo hivyo kwa kupiga simu ya bure 116.
Mwaka 2020 kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili, Serikali ilizindua programu hiyo tumizi GBV Taarifa jijini Dar es salaam nchini Tanzania wakati huu wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, tukio ambalo liliandaliwa kwa pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Tanzania na wadau wengine.
sheria ya mtoto ya mwaka 2009 imeainisha haki mbalimbali za mtoto ambazo jamii inapaswa kuzingatia, haki hizo ni pamoja na haki ya kutobaguliwa, haki ya kuwa na jina na uraia, haki ya kutunzwa na kukua akiwa na wazazi wake, haki ya maoni, haki ya kulindwa kutokana na mateso au adhabu zilizopitiliza. Ukiukaji wa haki hizi za mtoto zinaweza kupelekea aliyekiuka akitiwa hatiani, kulipa faini ya shilingi Milioni tano au kifungo cha miezi sita au vyote kwa pamoja.
Post A Comment: