Kamisa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 Anna Makinda akizungumza wakati akapokea taarifa ya utekelezaji wa zoezi la sensa ya watu makazi ya mwaka 2022 mkoani Tanga katika ziara yake Mkoani  humo kulia ini Mratibu sa Sensa Mkoa wa Tanga Tony Mwanjota kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Manyema 

Kamisa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 Anna Makinda akizungumza wakati akapokea taarifa ya utekelezaji wa zoezi la sensa ya watu makazi ya mwaka 2022 mkoani Tanga katika ziara yake Mkoani  humo kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba, Mratibu sa Sensa Mkoa wa Tanga Tony Mwanjota kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Manyema 
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba akizungumza kushoto ni Kamisaa wa Sensa nchini Anna Makinda kulia ni Mratibu wa Sensa mkoa wa Tanga Tony Mwanjoto
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema akizungumza
Mratibu wa Sensa Mkoa wa Tanga Tonny Mwanjota akieleza jambo


Na Oscar Assenga,TANGA.

KAMISAA nchini Anna Makanda amesema katika sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 watanzania walionyesha uzalendo mkubwa.


Makinda aliyasema hayo Jijini Tanga wakati akapokea taarifa ya utekelezaji wa zoezi la sensa ya watu makazi ya mwaka 2022 mkoani Tanga katika ziara yake Mkoani humo ambapo alisema uzalendo walionyesha wananchi unapaswa kuwa endelevu.


Alisema uzalendo huo ulitokana na wananchi katika maeneo mbalimbali nchini kupiga simu wakieleza bado hawajahesabiwa na hivyo kufikiwa na kuhesabiwa.


"Ndugu zangu Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 ilikuwa ya aina yake na watanzania walionyesha uzalendo wa hali ya juu "Alisema Kamisaa huyo


Hata hivyo alisema kwamba Rais Samia Suluhu ameweka nguvu kubwa kwa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama wamachinga na anasubiri baada ya kutangazwa matokeo ya sensa atafanya mambo yake ambayo ameyapanga.


Alisema kwamba Machinga ndio sekta ambayo inachukua watu wengi sana na nafasi ya machinga ni kubwa sana duniani na imekuwa na mchango mkubwa wa maendeleo.


"Hivyo kama utabaki umesomea udaktari wa binadamu basi unatakiwa ukatibie binadamu utapata matatizo tunategemea unaposoma unabadikika kutoka na mazingira yaliyopo kwa kuchangamkia fursa zilizopo"Alisema.


Katika hatua nyengine Kamisaa Makinda alisma kwamba wanatamani sana hiyo sensa itumie kwa ajili ya kuleta mabadiliko kwenye Jamii ikiwemo kuchapa kazi .


Hata hivyo alisema kwamba hivi sasa Serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania Bara (NBS) na Visiwani Zanzibar (OCGS) wanaandaa mpango wa mafunzo elimu kuhusu matokeo ya sensa ya watu na makazi yatakayotangazwa na Rais Samia Suluhu ili kila watu wafikirie na nafsi zao


Makinda alisema wamepanga kutumia takwimu zitakazopatikana kwenye Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kujiajiri ili kuondokana na tatizo la ajira hapa nchini.



Alisema ofisi ya Taifa has Takwimu ya Tanzania bara na Zanzibar wanaandaa mpango huo na takwimu zilizopatikana itabidi zifanye kazi mara baada ya Rais kuitangaza kutakuwa na program za kufundisha wananchi maana ya takwimu zile kusudi zitumike katika kazi zote kuanzia ngazi Vitongoji,Vijiji hadi Taifa lakini tunatamani sensa itumike katika mabadiliko" alisisitiza Makinda.


Awali akizungumza Mratibu wa Sensa Mkoa wa Tanga Tony Mwanjota alisema kuwa wameweza kufanikiwa kuhesabu kaya kwa asilimia 95 ikiwemo kuyafikia majengo yote ikiwemo kutoa elimu na hamasa kwa wananchi iliyosaidia ushirikiano wakati wa zoezi hilo wakiwemo viongozi wa Serikali ,Dini na Siasa .


"Tumeweza kufanikiwa kuhesabu kaya kwa asilimia 95 na kuyafikia majengo yote pia kuwezesha wananchi kuwa na elimu na hamasa ya kutosha kuhusu zoezi , mafanikio haya yametokana na viongozi wa dini serikali na sisasa , na kutokana na hamasa waliyokuwa nayo hatukutumia nguvu ya dola kumlazimisha mtu ahesabiwe bali wananchi wenyewe " alisema Mwanjota.


Aidha ameeleza baadhi ya changamoto walizokutana nazo makarani wa sensa zikiwemo ugumu wa kupata taarifa ikiwemo taarifa za uzazi na elimu kwa, kuchelewa kufika kwa vifaa kuletwa kwa mafungu pamoja na waratibu wa ngazi za wilaya kukosa mafunzo kikamilifu kutokana na zoezi la usaili wa makarani hivyo kushindwa kufikia lengo.


Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba alisema mkoa huo umeendele kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu ya kutenga maeneo kwa ajili ya kilimo ili kuifanya sekta hiyo iweze kuwakwamua wananchi na umasikini lakini pia kuwa na chakula toshelevu wakati wote ili kuweza kuchangia pato la Taifa.


Mkuu huyo wa mkoa alisema kwenye mkoa huo kuna uvamizi wa maeneo akieleza wameshatoa maelekezo ili waweze kutambua maeneo hayo wakiwemo wahusika waweze kupewa elimu na kuwaondoa ili kuepukana na migogoro ya ardhi.


Kwa mujibu wa Mratibu wa Sensa Mkoa wa Tanga Tony Mwanjota alisema katika sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 mkoa wa Tanga ulikadiria kuhesabiw jumla ya Kaya 649,591 lakini ni kaya 617,431 pekee zilizo hesabiwa na kufanya kufikia asilimia 95 huku sensa ya majengo ikifanikiwa kwa asilimia mia moja na hatimaye kuhesabu nyumba zipatazo 730,934.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: