Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amewataka wananchi wa kijiji cha Itumba wilayani Ileje Mkoani Mbeya kuhakikisha wanalinda vyanzo vya maji ili kuwezesha upatikaji endelevu wa huduma ya maji.
Aidha, amewahakikishia wananchi hao kuwa Serikali inaendelea na mipango ya kuhakikisha mradi wa maji Itumba-Isongole unakamilika ili huduma ya maji ifike katika maeneo yote ya kijiji hicho.
Mhe. Mahundi ametoa ahadi hiyo akiwa katika ziara ya kamati ya Mawaziri wa Kisekta katika kitongoji Cha Nkanka kijijini hapo.
Amesema nia ya Rais Samia ni njema na anatambua changamoto wanayopitia wananchi wa ileje.
"Niwahakikishie kuwa Mama Samia ana nia ya dhati ya kuhakikisha anawatua akina mama ndoo ya maji. Tuendelee kumuombea ili ndoto zake zitimie" Amesema Maryprisca.
Post A Comment: