Mjumbe wa Kamati ya Siasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Iddi Maalim (katikati) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kumi na nne  2022 ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Mtipa yaliyofanyika leo  Oktoba 22, 2022 katika viwanja vya shule hiyo iliyopo Manispaa ya Singida akikata keki ya upendo.  Kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Anna Mrisho. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Mtipa, Ramadhan Yusufu akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mtipa, Hamisi Mkenga.
Mkuu wa shule hiyo, Anna Mrisho, akitoa taarifa ya shule hiyo.
Viongozi mbalimbali wakiwakwenye mahafali hayo. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi wa shule hiyo, Athumani Shabani, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mtipa, Hamisi Mkenga.Diwani wa Kata ya Mtipa, Ramadhan Yusufu,Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida Iddi Maalim, Mwenyekiti wa Bodi wa shule hiyo, Mzee Wawa Lalli na Mkuu wa shule hiyo, Anna Mrisho,
Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wa kidato cha nne wakiimba wimbo maalum.
Wahitimu wa kidato cha nne wakionesha umahiri wa kutangaza habari
Wahitimu wa kidato cha nne  wakiimba shairi.
Keki ya Upendo ikipelekekwa eneo latukio.
Muonekano wa keki hiyo.
Wazazi na walezi wa wahimu hao wakiwa kwenye mahafali hayo.
Keki ikiliwa.
Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri katika michezo wakiwepo Kulwa na Dotto. 
Wahitimu wakimeremeta kwenye mahafali hayo.
Vyeti vikitolewa na mgeni rasmi.
Vyeti vikitolewa.
Furaha tupu kwa wahitimu hao.
Wafanyakazi wa shule hiyo wasio walimu wakitambulishwa kabla ya kukabidhiwa zawadi zao.
Mmoja wa wafanyakazi wasio walimu akipokea zawadi yake ambapo kila mmoja wao alizawadiwa shuka na foronya zake.

Na Dotto Mwaibale, Singida

WAHITIMU wa Kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Mtipa iliyopo Manispaa ya Singida wameaswa kutojiingiza kucheza kamari (kubet) kwani ni janga kubwa nchini.

Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Iddi Maalim ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kumi na nne  2022 ya kidato cha nne yaliyofanyika leo  Oktoba 22, 2022 katika viwanja vya shule hiyo na kuhudhuriwa na wazazi na wageni waalikwa kutoka shule jirani.

"Nchi yetu hivi sasa inashuhudia mambo ambayo hayapo hata kwenye dini vijana wetu wengi leo hii ukipita mijini utakuta wanashughulika na kitu kinaitwa kubeti au kucheza kamari hakika ili ni tatizo kwenye elimu wanabeti utafikiri watapata fedha" alisema Maalim.

Maalim alisema tangu ameanza kuwaona wakibeti hajawahi kushuhudia mtu akinunua nyumba yake zaidi ya kuambulia sH.100,000, SH.20,000 na elfu 10 huku akivutika na anaendeleakucheza analiwa na kurudi nyumbani akiwa hana kitu.

Alisema mchezo huo umtengenezwa na walioubuni ili kuchota pesa kutoka kwetu hivyo anapenda kusisitiza kuwa hauna faida na wasidanganyike kwani inawanufaisha wale walioutengeneza kwa kutumia mahesabu makali.

Akizungumzia masuala ya elimu alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa elimu bila ya malipo pamoja na kutoa fedha nyingi kuboresha miundombinu ya shule mbalimbali hasa ujenzi wa vyumba vya madarasa kote nchini na Shule ya Sekondari ya Mtipa ikiwa ni moja ya shule iliyonufaika kwa kupata madarasa saba..

Maalim alitumia nafasi hiyo kuwaasa wahitimu hao waangalie mifano iliyopo ya viongozi au watu mashuhuri waliojituma na kufanya kazi kwa bidii kwenye elimu na kwenye maisha na akawata wajifunze kutoka kwao.

Aidha Maalim aliwata wahitimu hao kuwaenzi wazazi wao kwa kusoma kwa bidii huku wakifuata nasaha zao juu ya kujiheshimu, kujitunza na akawaomba wazazi wasichoke kuwahimiza watoto wao kwenda shuleni ikiwa ni pamoja na kupitia madaftari yao kuona kile wanachofundishwa.

Mkuu wa shule hiyo Anna Hamphrey Mrisho alisema shule hiyo licha ya kuwa na changamoto za hapa na pale kama upungufu wa walimu na mambo mengine alitaja baadhi ya mafanikio kuwa ni pamoja na kupokea fedha kutoka Serikalini kuu Sh.140,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa uyumba saba vya madarasa.

Alitaja mafanikio mengine ni kuwawezesha wanafunzi kujitambua kuhusu maisha yao, robo tatu ya wanafunzi kuweza kukaa kambi ya masomo kwa miezi mitatu ili kuinua taaluma yao, kupata nishati ya umeme kwenye vyumba viwili katika jengo la utawala, kuborsha ofisi ya mkuu wa shule na kukamilisha vyumba vyote vya maabara.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: