Mkuu wa wilaya ya Ikungi Jerry C. Muro leo akiambatana na viongozi wa kamati ya usalama ya wilaya pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi wamefanya ziara ya kutembelea shamba la mwekezaji kampuni ya Alfadaws investment company kutoka Jordan ambao wamewekeza kwenye kilimo cha alizeti katika shamba la hekari 1,700 katika kata ya mkiwa kijiji cha choda
Katika ziara hiyo Dc Muro amepata nafasi ya kusikiliza kero na changamoto anazokabiliana nazo mwekezaji na kutembelea eneo ambalo limeshasafishwa tayari kuanza msimu mpya wa kilimo kwa mwaka 2023
Akitoa taarifa kwa wajumbe, msimamizi wa mradi huo Ndugu Anas amesema katika mradi huo wanatarajia kulima alizeti kwa mfumo wa umwagiliaji wa kisasa na wanatarajia kujenga kiwanda kikubwa cha kukamulia alizeti kwa mtindo wa kisasa, pamoja na kuzalisha mbegu kwa ajili ya soko la ndani na nje ikiwemo kusaidia wazalishaji wa alizeti nchini na kusisitiza wamejipajga kuanza kulima katika msimu huu
Dc Muro kwa upande wake amewahakikisha wawekezaji hao wanaendelea kutatua changamoto ikiwemo ukamilishaji wa mchakato wa kuwapatia hati, kukarabati barabara inayoelekea kwenye mradi
Post A Comment: