Na Gift Mongi

Moshi


Licha ya moto uliozuka octoba 21 katika eneo la hifadhi ya mlima Kilimanjaro kudhibitiwa mapema baadhi ya wadau wamependekeza jitihada za maksudi zifanyike ili kuweza kukabiliana na tatizo hilo pindi linapojitokeza.


Katika zoezi hilo baadhi ya makundi mbalimbali yalishiriki kuukabili ambapo pia vijiji vya jirani na wenyewe waliweza kushiki kwa aina moja ama nyingine katika kukabiliana na moto huo kabla madhara zaidi hayajajitokeza.


Mwenyekiti wa umoja wa chama cha mapinduzi(UVCCM)wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenali Shirima ni miongoni mwa viongozi walioongoza mapambano katika kuuzima moto huo uliozuka katika eneo la Karanga kuelekea Baranko umbali wa mita 3,963 kutoka usawa wa bahari.


Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo ni kuwa mlima Kilimanjaro umekuwa ni kivutio kinachoitangaza Tanzania lakini pia kinalingizia fedha za kigeni na ndio maana lililopojitokeza suala la moto ilikuwa ni rahisi kuhamasisha kundi la vijana katika kwenda kuongeza nguvu kutokana na umuhimu uliopo.


Shirima anasema kuwa wastani wa watalii zaidi ya 230 hupanda mlima huo kupitia malango sita yaliyopo katika mlima huo na kufanya wastani wa watalii 7000 kwa mwezi hivyo kuathirika kwa mlima huo kungeweza kuleta athari katika sekta nzima ya utalii.


Anasema kwa sasa ipo haja kuendelea kuona namna ya kujipanga kwa kuwepo na vitendea kazi vya kisasa katika kupambana na moto kwani imeshaonekana ni tatizo ambalo hujirudia mara kwa mara hivyo ni vyema kujiandaa mapema.


Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo amewataka vijana kujitolea katika ulinzi wa rasilimali zetu kwani zina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa lakini pia ukuaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo kama afya maji,barabara na elimu.


Ameongeza kuwa hategemei kuona vijana wakishindwa kulinda rasilimali hizo na kuwa kama zisingelindwa kwa miaka ya nyuma leo hii zisingekuwepo na kuwa ni wajibu wao kufanya hivyo kwani hakuna mtu anaweza kutoka nchi nyingine aje awe mlinzi katika taifa lako.


Gervas Munisi ni miongoni mwa vijana walioshiriki katika zoezi hilo ambapo amesema wameweza kufanikisha kutokana na umoja uliokuwepo na kuwa nguvu kazi ilikuwepo yakutosha lakini pia vijana walionekana kujitolea kwa mali na mali.

Share To:

Post A Comment: