Na John Walter-Babati
Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange amesema vitendo vya ukatili ndani ya mkoa wa Manyara ni jambo la fedhea na linarudisha nyuma taswira ya mkoa wa Manyara.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Manyara katika kilele cha maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kilichofanyika katika kijiji cha Mandi kata ya Dabili wilayani Babati Twange ameahidi kukomesha vitendo hivyo.
Naibu katibu mkuu wizara ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum Amon Mpanju amewaomba wadau mbalimbali hapa nchini kuiunga mkono serikali katika kupambana na vitendo vya ukatili kwa lengo la kutengeneza jamii yenye matokeo chanya.
Kampeni ya kupinga ukatili ni kampeni inayofanyika nchi nzima kwa lengo la kupinga vitendo vya kikatili katika jamii.
Post A Comment: