Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi-Uchukuzi Mhe.Atupele Mwakibete akipata maelezo kutoka kwa Afisa udhibiti ubora wa TBS Bw.Tumaini Chimangha alipotembelea banda la TBS kwenye Maonesho ya Wabunifu Majengo na Wakadiliaji Majenzi yaliyofanyika leo Oktoba 19,2022 katika Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi-Uchukuzi Mhe.Atupele Mwakibete akipata maelezo kutoka kwa Afisa udhibiti ubora wa TBS Bw.Tumaini Chimangha alipotembelea banda la TBS kwenye Maonesho ya Wabunifu Majengo na Wakadiliaji Majenzi yaliyofanyika leo Oktoba 19,2022 katika Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
**********************
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeshiriki katika Maonesho ya Wabunifu Majengo na Wakadiliaji Majenzi yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika Maonesho hayo leo Oktoba 19,2022 Jijini Dar es Salaam, Afisa udhibiti ubora wa TBS Bw.Tumaini Chimangha amesema TBS limeshiriki kwenye Maonesho hayo ili kuwapatia elimu ya viwango wabunifu Majengo na Wakadiiliaji Majenzi ili majengo ambayo wanayabuni yawe bora na yenye viwango.
Amesema kuna umuhimu mkubwa kwa wabunifu majengo kuelewa na kufuata taratibu za viwango vya matumizi ya vifaa vya kupimia majengo ambayo wamekuwa wakiyabuni na kuondoa kasoro ambazo zingeweza kuleta athari kwenye majengo ambayo yatajengwa.
Aidha amesema ushiriki katika maadhimisho hayo ni mkubwa kwani wabunifu mbalimbali wa majengo wameweza kutembelea banda la TBS na kupewa elimu juu ya matumzi sahihi ya viwango.
Post A Comment: