Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bi.Rehema Madenge akizungumza katika ufunguzi mafunzo ya Utekelezaji wa kanuni za Ushirikiano katika Utekelezaji wa Mamlaka na Majukumu baina ya TBS na Tamisemi yaliyotolewa kwa Maafisa Afya na Maafisa Biashara wa mkoa wa Dar es salaam. Kaimu Mkurugenzi Mkuu TBS, Dkt.Candida Shirima akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya Utekelezaji wa kanuni za Ushirikiano katika Utekelezaji wa Mamlaka na Majukumu baina ya TBS na Tamisemi yaliyotolewa kwa Maafisa Afya na Maafisa Biashara wa mkoa wa Dar es salaam.
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SHIRIKA la Viwango Tanzania limefanya mafunzo ya Utekelezaji wa kanuni za Ushirikiano katika Utekelezaji wa Mamlaka na Majukumu baina ya TBS na Tamisemi yaliyotolewa kwa Maafisa Afya na Maafisa Biashara wa mkoa wa Dar es salaam.
Akizungumza wakati akifungua Mafunzo hayo leo Oktoba 4,2022 Jijini Dar es Salaam, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bi.Rehema Madenge amesema mafunzo hayo ni njia muafaka ya kuleta tija zaidi katika juhudi za kuleta maendeleo katika udhibiti wa bidhaa za chakula na vipodozi katika mkoa huo na Taifa kwa ujumla.
Amesema Serikali imeazimia kwa dhati kuendeleza biashara kwa kuhakikisha bidhaa za chakula na vipodozi zinakidhi matakwa ya viwango vya ubora na usalama.
"Nitoe rai kwenu nyie watumishi wa Serikali kuwa majukumu tuliyopewa yawe chachu ya sisi kutumikia umma kwa bidii bila ubaguzi, kuwashauri na kuwasaidia kitaalamu pale inapohitajika (tusibweteke), ili bidhaa zetu ziwe bora na salama na uchumi wetu uendelee kukua". Amesema Bi.Madenge.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu TBS, Dkt.Candida Shirima amesema ili kuimarisha mfumo wa udhibiti wa usalama wa chakula na vipodozi katika ngazi zote nchini kwa lengo laa kulinda afya ya jamii, mwaka 2021 zilitungwa kanuni za ushirikiano katika utekelezaji wa mamlaka na majukumu baina yaa TBS na TAMISEMI.
"Kanuni hizi zilitungwa kwa kuzingatia mamlaka aliyopewa Waziri mwenye dhamana ya Viwanda na Biashara chini ya sheria ya viwango, Sura 130". Amesema
Aidha amesema lengo lakutunga kanuni za kushirikisha baadhi ya madaraka na majukumu ya tbs kwa Halmashauri ni pamoja na kusogeza karibu wananchi huduma za udhibiti wa ubora na usalama wa chakula na vipodozi na kuwa na mtandao ndani ya nchi nzima katika shughuli za udhibiti wa bidhaa hizo.
Post A Comment: