DENIS CHAMBI, TANGA.
Katika kuendelea kuwaelimisha na kuwarahisishia wananchi juu ya huduma ya Nikonekt ya shirika la umeme Tanzania 'TANESCO' mkoa wa Tanga imtoa mafunzo maalum ya ubalozi kwa waandishi wa habari wakiwa ni wadau muhimu katika shirika hilo ili kuendelea kuhabarisha jamii kupata huduma zilizo Bora sambamba na kuwasaidia kuondokana na ulaghai wa watu ambao wamekuwa wakiwatoza fedha kwa maslahi yao binafsi.
Akizungumza mara baada ya kutoa mafunzo hayo afisa uhusiano na wateja kutoka shirika la umeme Tanzania 'TANESCO' mkoa wa Tanga Amoni Bidebuye alisema kuwa kwa kutambua mchango wa vyombo vya habari hapa nchini katika sekta hiyo kupitia huduma zinazotolewa na Tanesco wameona ipo haja kuwatumia waandishi wa habari ili kuwafikia wananchi popote walipo kuendelea kurahisisha uboreshaji, upatikanaji na utoaji wa huduma ambamba na kupambana na uharibifu wa miundombinu.
"Tunataka waandishi wa habari wawe mabalozi katika mfumo wa uboreshwaji wa uunganishaji wa umeme 'Nikonekt' tunataka taarifa imfikie mteja popote pale alipo ili angalau kila mwananchi afahamu na aelewe Tanesco ipoje sasa, tumekubaliana kila mmoja atakuwa balozi , kutoa elimu ya namna wateja watapata huduma kupitia mfumo wa kidijitali wa Nikonekt ambao hauna haja ya kufika Tanesco ili upate huduma"
"Na hii huduma ya Nikonekt imekuja kutatua changamoto kubwa iliyokuwa ikiwasumbua wateja wetu ambayo ilikuwa ili upate huduma lazima uwe na mtu pale Tanesco au lazima utumie mtu yeyote wa kati sasa Nikonek tukasema hapana unaweza ukapata huduma ukiwa hata nyumbani tunataka wananchi wajue kuwa sasa hivi kuunganishiwa umeme sio suala la kuwa unamfahamu nani" aliongeza Bidebuye.
Aidha afisa huyo alisema katika kuendelea kupambana na kutatua changamoto ya uharibifu wa miundombinu ya umeme wameona ni vyema kuwatumia wanahabari katika kupata taarifa na kutoa elimu kwa wananchi juu ya ulinzi wa miundombinu ili kuwa salama nyakati zote na kuendelea kutoa huduma.
"Lakini kubwa zaidi pia tumekubaliana kuwa mabalozi wa usalama wa miundombinu kwa sababu imeonekana moja ya tatizo linaloleta changamoto kwenye suala kukatika kwa umeme ni kutokana na uharibifu wa miundombinu mtu akivamia na kuingilia umeme tayari umeme unakatika"
Afisa uhusiano huyo alibainisha kuwa huduma hiyo ya Nikonekt imekuja kuleta mafanikio makubwa na kuondoa malalamiko tofauti na hapo awali kwani mara tu mteja anapokamilisha taratibu zote za kuomba huduma ya kuunganishiwa umeme taarifa zimekuwa zikiwafikia Tanesco na ndani ya siku tatu mwamachi hupatiwa huduma yake.
Akizungumzia suala la kutakika katika kwa umeme mara kwa mara alisema mabadiliko ya tabia nchi yamechangia kwa kaisi kikubwa ikiwa ni pamoja na kukauka kwa mto uliopo Hale unaopeleka maji katika Bwawa la Pangani ambapo amesema kuwa katika kupambana na changamoto hiyo zipo jitihada zilizoendelea kufanyika ikiwa pamoja na kukarabati miundombinu iliyopo.
" Kuna miradi mbalimbali inaendelea kufanyika hapa nchini lakini sisi kama Tanga tunahakikisha kuwa muda huu tunatumia kufanya matengenezo na tunatarajia muda sio mrefu tuwe tumemaliza matengenezo ya njia zetu isije ikatokea tena mtu anakatiwa umeme ,na tunaendelea kufanya ukarabati na kuimarisha ulinzi maana mengine yanasababishwa na shughuli za kibinadamu mfano wanaolima karibu na miundombinu" alisema Bidebuye.
"Lakini pia mabadiliko ambayo tunatarajia kuyafanyia ni kuchukua umeme kutokea Arusha kuja Tanga kama hii hali ya kukatika katika kwa umeme itaendelea na hivyo kufikia mwezi wa kumi na mbili hadi wa kwanza na hiyo itasaidia kuongeza kiwango cha umeme wa kutosheleza kwa mkoa wa Tanga" alisema Bidebuye.
Wakizungumza baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kupata elimu hiyo ya kuwa mabalozi wa Tanesco walisema kuwa kwa kutumia taaluma na kalamu zao wapo tayari kuelimisha wananchi kuhusu huduma zinazotolewa na shirika hilo pamoja na kushirikiana katika kulinda na kutunza miundombinu ya umeme katika maeneo mbalimbali.
"Kwa kupitia kwetu sisi waandishi wa habari maswala mengi sana yataeleweka kwasababu moja wapo ya matatizo ambayo yamekuwa yakitokea ni ukosefu wa elimu na taarifa na hazifiki sehemu zinakotakiwa lakini sasa kwa kupitia vyombo vya habari itatusaidia kwa kiasi kikubwa kufikisha taarifa nasisi kwa kutumia utaalamu wetu katika kuwaelimisha watu" alisema George Semboni Mwandishi wa gazeti la Citizen.
" Sisi kama mabalozi wa Tanesco hapa nchini na hasa mkoa wa Tanga tunapongeza jitihada zinazofanyika kuboresha upatikanaji wa umeme na tunajua kabisa kwamba umeme ni tegemeo kubwa na mkoa wa Tanga unakuwa ni tegemeo kubwa na fursa zote zipo tunaona kuna Barabara kubwa inatengenezwa ya kutoka Bagamoyo hadi Tanga ujio wa Bomba la mafuta, upanuzi wa bandari ya Tanga kwa hivyo umeme ni nyenzo muhimu sana ya kukuza uchumi wa mkoa na Taifa" alisema Willium Mngazija mwandishi wa ITV.
MWISHO.
Post A Comment: