DENIS CHAMBI, TANGA.

Serikali kupitia tume za taifa za Takwimu Tanzania  bara 'NBS'  na visiwani Zanzibar 'OCGS' imelenga  kutumia takwimu za watu zilizopatikana kwenye Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022  kutoa elimu kwa umma  juu ya umuhimu wa kujiajiri ili kuondokana na tatizo la ajira hapa nchini.


Hayo yamebainishwa na kamisaa wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 mkoani Tanga Anne  Makinda  wakati alipokuwa akipokea taarifa ya utekelezaji wa zoezi la Sensa ya watu na makazi ambalo  lilifanyika Augost 23 mwaka huu  ambapo  amebainisha kufanikiwa kwa zoezi hilo zaidi  ya asilimia 90 kote nchini hii ikiwa ni kutokana na elimu iliyotolewa kwa wananchi ambao wameonyesha ushirikiano kwa makarani wa sensa kote nchini.


"Ofisi zetu  ya takwimu  Tanzania bara na  Zanzibar  wanaandaa mpango wa kutoa elimu kuhusu matokeo ya sensa ilivyofanyika,takwimu zilizopatikana itabidi zifanye kazi  mara baada ya Rais kuitangaza kutakuwa na program za kufundisha  wananchi maana  ya tawimu zile kusudi zitumike  katika kazi zote kuanzia ngazi kitongoji na hadi Taifa , ikiwemo taarifa za ni wapa hakuna huduma za kijamii tunatamani sana hii sensa itumike katika mabadiliko" alisema Makinda.


"Takwimu zetu safari hii tunataka zifanye kazi , mheshimiwa Rais ameweka nguvu kubwa sana kwa wamachinga , machinga itakuwa ndio sekta ambayo itachukuwa watu wengi sana hivyo katika sensa hii kuna kila kitu kuna mahali inaonyesha kabisa vijana wetu waliosoma na wapo nyumbani kwa muda mrefu  , ugonjwa tulio nao sisi sio kazi hazipo bali tuna ugonjwa  wa tafsiri elimu sio kuajiriwa bali ni ufunguo wa maisha" alieleza.


Awali akieleza namna sensa ilivyofanyika kwa mkoa wa Tanga mratibu  wa mkoa huo Tony Mwanjota alisema kuwa wameweza kufanikiwa kuhesabu kaya kwa asilimia 95 na kuyafikia majengo yote, kuiwezesha kutoa elimu na hamasa kwa wananchi  ambayo imepelekea ushirikiano mkubwa uliochangiwa na viongozi wa  serikali dini na siasa .


"Tumeweza kufanikiwa kuhesabu kaya kwa asilimia 95 na kuyafikia majengo yote  pia kuwezesha wananchi  kuwa na elimu na hamasa ya  kutosha  kuhusu zoezi , mafanikio haya  yametokana na  viongozi wa dini serikali na sisasa , na kutokana na hamasa waliyokuwa nayo hatukutumia  nguvu ya dola  kumlazimisha mtu  ahesabiwe  bali wananchi wenyewe " alisema Mwanjota.


Aidha ameeleza baadhi ya changamoto walizokutana nazo makarani wa sensa  zikiwemo ugumu wa kupata taarifa ikiwemo taarifa za uzazi  na elimu kwa, kuchelewa kufika kwa vifaa kuletwa kwa mafungu pamoja na   waratibu  wa ngazi za wilaya  kukosa mafunzo kikamilifu kutokana na zoezi la usaili wa makarani hivyo kushindwa kufikia lengo.


Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba  ameeleza kuwa  wanaendelea kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan  ya kutenga maeneo maalumu  kwaajili ya kilimo ili kutumia sekta ya Kilimo katika kuwakwamua wananchi na umasikini na kuwa na chakula toshelevu wakati wote ili kuweza kuchangia pato la taifa.


"Tunaendelea kuyafanyia kazi maelekezo ya Rais aliyosema tutenge kila mkoa hekali zisizopungua laki moja na hamsini kwaajili ya kilimo hususani mazao yale ambayo tunakwenda zinazotukabili katika  taifa letu mfano mazoa yenye asili ya mafuta maeneo hayo tayari tumeyatenga na tumeshazielekeza ofisi zetu za wilaya kutenga maeneo hayo " alisema Mgumba.


"Kuna uvamizi wa maeneo lakini tumeshatoa maelekezo tuyabaini hayo maeneo na watu husika tuwape elimu na kuwaondoa  na kwababu hili linakuja sambamba na migogoro ya ardhi katika mkoa wetu ikiwemo wananchi kuvamia  maeneo ya viwanda na uwekezaji"


Katika sensa ya watu  ya mwaka 2022 mkoa wa Tanga ulikadiria kuhesabiw jumla ya Kaya 649,591  lakini ni kaya 617,431 pekee zilizohesabiwa  na kufanya kufikia asilimia 95 huku  sensa ya majengo ikifanikiwa kwa asilimia mia moja na hatimaye kuhesabu nyumba  zipatazo 730,934. 

Share To:

Post A Comment: