Na Mwandishi wetu Mbeya 

HATIMAYE  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amevunja ukimya na kutolea ufafanuzi juu ya kauli yake ya ‘nyooka naye’ inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii. Dkt. Tulia anasema anayesambaza kipande hicho cha video ana nia ovu dhidi yake.

Akizungumza mara baada ya kufungua kongamano la wanawake wachungaji wa Kanisa la Moravian Tanzania lililofanyika jijini Mbeya, Dkt. Tulia amesema kipande kilichokamilika kipo na ikiwa mtu atapenda kupata taarifa kamili anaweza kuifuatilia lakini siyo kusambaza habari za uongo ambazo zinaleta taharuki katika jamii.

“Asitokee mtu yeyote…wa nje ya chama, wa ndani ya chama akawa anamsema vibaya Rais halafu wewe ukawa unamtazama…shughulika naye…hata mimi Mbunge wako nikiwa ninasemwa vibaya …nyooka naye…” haya ni baadhi ya maneno yanayosikika katika kipande hicho cha video kinachosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Dkt. Tulia ameeleza kwamba “Ile taarifa ipo kamili, ni mtu tu ameamua kuchukua kipande anachokitaka kwahiyo hakuna maelezo ya ziada zaidi ya yale na wala hakuna jambo lolote lililosemwa pale ambalo mtu anaweza kusema pengine limesemwa kwa namna isiyo stahili.. hapana! Vile ndivyo ilivyopaswa kuwa”

“Wale wanaoambiwa pale lazima utetee hoja, hata mimi natetea hoja na hizo ni lugha za kawaida kabisa na hilo wala hazinishangazi. Wao wanatafuta jambo baya na wameona namna bora ni kukata kipande lakini kipande kizima kipo na wanaohitaji kukisikiliza watakisikiliza”- Amesisitiza Dkt. Tulia

Share To:

Post A Comment: