Wananchi wa vijiji 8 katika kata ya Sepeko na Lepurko ambao wameathirika na ukame kwa kukosa huduma ya maji wamepata Neema ya msaada wa Maji kutoka Serikalini.
Haya yanajiri siku chache baada ya Mtandao huu kuripoti hali mbaya ya ukosefu wa maji navyowakumba wanafunzi wa Nanja Sekondari ambapo Mbunge wa Jimbo la Monduli Fredrick Lowassa, akiwa ameongozana na Waataalamu wa maji (RUWASA) Kutoka Mkoa wa Arusha amefika Eneo la Bwawa la Nanja nilalotumiwa na wanafunzi hao sambamba na kata mbili ili kujionea maji yalikuwa yakilalamikiwa na wananchi kuwa si salama ili kutafuta Mpango wa Dharura wa kuwasaidia Wananchi hao.
"Huu mpango ni Wa Dharura kuwasaidia angalau kwa Kila Kijiji kuweka simtank mawili , Vijiji vilivyoathirika zaidi ni Vijiji 8 , Mtimmoja, Arkaria,Arkatan, Losimingori, Nanja , Mbuyuni, Lepurko na Engarooji kutoka kata ya Sepeko na Lepurko , Mpango huu Serikali imetoa shilingi Millioni mia moja kwa ajili ya kununua Simtank na kuweka maji kwa ajili ya matumizi ya kibinadamu lakini Kuna ule mradi mkubwa wa maji na vijiji 13 Vitanufaika na Mradi huo" Mbunge Fredrick Lowassa
" Changamoto hatuzijibu kwa maneno tunajibu kwa vitendo lakini pia ni vizuri watu wakafahamu mabadiliko ya tabia ya nchi, Leo hii Mwaka Jana changamoto kubwa ya maji ilikuwa kubwa lakini yote haya ni mabadiliko ya tabia ya nchi kwa sababu tungekuwa na mvua ya kutosha Hili Bwawa lingeweza kusaidia, mabadiliko ya tabia ya nchi sio nje ulaya peke yake hata Afrika linatukumbuka ,vyanzo vya maji vimekauka , kwa hiyo Kuna namna ya kujali namna ya kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi, Niishukuru Sana Serikali kupitia kwa Waziri wa Maji Juma Aweso nilimpigia simu kumeelezea tatizo la Maji Monduli na aliniahidi kulifanyia kazi na kazi yake tumeiyona".
Kwa Upande wake Meneja wa RUWASA Mkoa wa Arusha Joseph Emmanuel Makaidi amesema maeneo hayo ni maeneo ambayo hayana maji juu ya Ardhi , na utafiti wa kipindi Cha nyuma ilionyesha kuwa maeneo haya ni maeneo ambayo hayana maji chini ya Ardhi.
"Kama Mbunge alivyosema aliwasilisha ombi Hili Wakati wa Kampeni na mara moja tukaagizwa tutengeneze mpango wa kuipatia maji maeneo kame haswa ya Wilaya ya Monduli"
Mpango ukafanyika na Serikali ikatoa pesa kwa ajili ya kupeleka maji Monduli mjini pia katika Vijiji 13 ambayo hayana maji juu ya Ardhi na hata chini ya Ardhi". Eng Makaidi
Post A Comment: