DENIS CHAMBI, TANGA.
Serikali imetoa kiasi cha shilingi million mia mbili kwaajili ya ujenzi wa mabweni mawili ya wanafunzi 160 wa kiume na wakike wa shule ya Sekondari Funguni iliyopo wilaya ya Pangani mkoani Tanga yanayotarajiwa kukamilika Desember, 2022.
Akizungumza kwenye mradi huo mkuu wa wilaya hiyo Ghalibu Lingo amesema kuwa mara baada ya kupokea fedha hizo walikubaliana na wananchi kushiriki katika kuongeza nguvu kazi ili mradi huo uweza kukamilika kwa wakati ambapo utakwenda kutatua changamoto ya wanafunzi kukosa masomo kutokana na sababu mbalimbali pamoja na kuongeza kiwango cha ufaulu.
"Wananchi tuliwapa elimu ya kutosha kuwatawaambia kwamba fedha anazozitoa rais wetu za sekta za huduma ziwe ni Chachu ya maendeleo na zinazotufanya sisi tuweza kukamilisha majengo hayo"
"Fedha zilizotolewa na Serikali ni shilingi milioni Mia mbili lakini tukizipigia tathmini fedha hizo haziwezi kumalizia mradi maana ni pamoja na vitanda hivyo tumekaa na wananchi kujaribu kuangalia kwa kujenga kwa force akaunti tumekubaliana kwa pamoja Kuna kazi nyingine zinatakiwa zifanywe na wananchi lakini zitathminiwe kma tungelipa fedha ingekuwa ni kiasi gani lakini hawa ndio wanofanya kazi ya kuchimba msingi, kuweka zege ni sehemu ya mchango ili helainayobaki iweze kumalizia adhima ya kutengeneza" alisema Ringo
Akizungumza suala la utoro kwa wanafunzi alisema kuwa wameweka sheria ndogo ndogo kwa kushirikiana na wazazi kupambana na suala la utoro wa wanafunzi mashuleni
"Kukabiliana na suala la utoro tumeweza kuangalia namna ya kubadilisha utawala mashuleni, kupika chakula cha mchana hali ambayo inamfanya mwanafunzi asitoroke lakini kwa kushirikiana na wananchi tumetengeneza sheria ndogo ndogo na tumekubaliana kila mzazi ahakikishe mtoto wake anaenda shule na matokeo nayo yanavutia kumfanya mtoto asiwe mtoto" alisema.
Aidha Lingo amewataka wananchi wa wilaya hiyo kushirikiana kulinda miundo mbinu mbalimbali inayotekelezwa katika wilaya hiyo kuilinda ili iweze kuendelea kutoa huduma kwao na kwa maslahi mapana ya kizazi kijacho.
Diwani wa kata Pangani Mashariki ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya fedha ya halmashauri ya wilaya hiyo Akida Boramimi aliishukuru serikali kwa kuridhia na kutoa fedha hizo ambazo zinakwenda kutatua changamoto ya wanafunzi wanaotembea umbali wa kilomete 4.
" Mradi huu unatakiwa kukamilika mwezi December mpaka sasa hatuna changamoto yeyote ya vifaa vya ujenzi wa mradi mpaka sasa wadau mbalimbali na kupitia nguvu za wananchi ndio fedha ambayo tunaendelea nayo na hata hiyo million Mia mbili iliyotolewa na serikali bado hatujaitumia" alisema Boramimi
"Tunamshukuru Sana rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiona wilaya yetu, ukamilika kwa mradi huu kitasaidia wanafunzi Safari ya kwenda na kurudi tuna kata tatu wanafunzi kwa ng'ambo ya Bweni wanatembea umbali wa kilomita nne kwahiyo ikiwepo hosteli hapa watapata muda mzuri wa kujisomea na Ile changamoto ya kutembea zitakuwa zimewapungukia," aliongeza
Kwa upande wao wananchi walioshiriki katika msaragambo wa ujenzi huo kwa hatua za awali walizungumzia utayari wao wa kuweza kushiriki na kuchangia kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo elimu ili kuendelea kuongeza huduma mbalimbali za kijamii katika wilaya hiyo.
"Sisi wananchi wa tumehamasika sana kwenye suala la elimu kuchangia nguvu zetu na kuniunga mkono rais wetu kwa msaada wa hali na mali tunafanya kazi kwa mapenzi yetu hatukulazimishwa ombi letu kwa serikali tunaomba watuongezee miradi mingine tupo tayari kujitolea " walisema wananchi hao.
Nje ya fedha hizo kwaajili ya ujenzi wa mabweni mawili ya wilaya ya Pangani pia imepokea shilingi milioni 200 kwaajili ya ujenzi wa madarasa kumi , matano yakijengwa katika shule hiyo ya Sekondari Funguni yatakayotumiwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023.
Post A Comment: