Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ruvu mkoani Pwani wakiwa wamebeba keki iliyotolewa na wanafunzi waliosoma katika shule hiyo kuanzia mwaka 1977 hadi sasa ikiwa ni ishara ya kuzindua Kampeni ya ujenzi wa kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga uzio wa Shule hiyo ili kuimarisha usalama wa wanafunzi wa kike.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Ruvu mkoani Pwani Juliana Chimanzi (wa tatu kulia) akiwa na baadhi ya walimu waliofundisha katika shule hiyo( walioko kulia) wakiwa na baadhi ya wanafunzi waliosoma shuleni hapo kuanzia mwaka 1977 wakikata keki kuashiria uzinduzi wa Ujenzi wa uzio wa Shule hiyo .Wanafunzi hao wameamua kuchangishana fedha ili kusaidia kununua sehemu ya vifaa vya ujenzi na kukabidhi kwa uongozi wa Shule hiyo jana.
Zawadi zikitolewa.

Victoris Massawe( wa pili kulia) ambaye ni moja ya wanafunzi waliosoma katika Shule ya Ruvu Sekondari ambaye pia ni mmoja ya Waratibu wa michango ya wanafunzi akikabidhi tofali kwa Waziri MKuu wa Wanafunzi wa Shule hiyo Minael Katamba (kushoto) jana baada ya wanafunzi waliosoma kwenye shule hiyo kuanzia mwaka 1977 mpaka sasa kuamua kuchangia vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa uzio wa Shule hiyo.

Baadhi ya wanafunzi walisoma katika Shule ya Sekondari Ruvu mkoani Pwani kuanzia mwaka 1977 hadi sasa wakiwa na baadhi ya wanafunzi walioko sasa pamoja na walimu wakiwa wameshika moja ya tofali kuashiria makabidhiano ya vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa uzio wa Shule hiyo ambayo kwa sasa ni ya wanafunzi wa kike peke yake.Vifaa vya ujenzi matofali na nondo vimekabidhiwa shuleni hapo na wanafunzi waliosoma kwenye shule hiyo kuanzia mwaka huo ambao wameamua kuchangishana fedha kusaidia sehemu ya uzio wa Shule.
 Mwenyekiti wa Wanafunzi waliosoma kwenye shule hiyo,  Veronica Chambuso akizunguza katika tukio hilo. 
Dada Mkuu wa Shule ya Sekondari Ruvu Jacquline Mgisha, akuzungumza katika tukio hilo.

 Wanafunzi wa kwanza kabisa kuanza kusoma katika Shule ya Sekondari Ruvu iliyopoanza  mwaka 1977 wakijitambulisha kwa wanafunzi na walimu walioko sasa baada ya kufika shuleni hapo kwenye tukio la kukabidhi vifaa vya ujenzi nondo na matofali ili kuanza ujenzi wa uzio wa Shule hiyo.


 Na Mwandishi Wetu, Pwani


UONGOZI wa Shule ya Ruvu Sekondari umesema kiasi cha Sh.milioni 794.9 kinahitajia kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa uzio shule hiyo kwa lengo la  kuimarisha usalama wa wanafunzi wa kike 850 wanaosoma kwenye shule hiyo. 

Akizungumza jana wakati wa tukio la upokeaji wa vifaa vya ujenzi (matofali na nondo) vilivyotolewa na wanafunzi waliosoma shule hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 1977 mpaka sasa,  

Mkuu wa Shule ya Ruvu Sekondari Juliana Chimanzi alisema uzio wa shule ni muhimu kwani kuna changamoto ya mifugo kuingia eneo la shule lakini pia wezi na vibaka. 

"Nitoe  Serikali, wadau na kwa namna ya kipekee wanafunzi waliopita hapa kokote waliko watusaidie.Shule yetu ina idadi kubwa wanafunzi wasichana ambao wanafikia 850 , tunahitaji kuweka ulinzi kwa kujengewa uzio.Tumefanya tathimini Sh.Sh.milioni 794.9 zinahitajika,”aamesema. 

Awali akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo vya ujenzi, Mwenyekiti wa Wanafunzi waliosoma kwenye shule hiyo kwa nyakati tofauti Veronica Chambuso kuanzia mwaka 1977 amesema wameona wachangishane ili peleka vifaa vitakavyosaidia kuanza ujenzi wa uzio. 

“Tumeleta matofali na nondo , huu ni mwanzo lakini tunaendelea kuwaomba waliosoma Ruvu Sekondari kuanzia mwaka 1977 mpaka sasa na miaka inayokuja, wazazi , wafadhili na wale wanaoguswa na ulinzi wa watoto wa kike tushirikiane kwani ukimlinda mtoto wa kikekwani  akapata elimu itamsaidia na taifa litanufaika,”alisema Chambuso. 

Amefafanua kwamba  shule hiyo ilijengwa mwaka 1977 baada ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kuomba msaada Serikali ya Cuba, hivyo wanamshukuru kwa upendo wake na katika kumuenzi wameona kuna uhitaji mkubwa wa uzio. 

Kwa upande wao Waratibu wa Uchangiaji huo ambao nao ni sehemu ya wanafunzi waliosoma shule hiyo Devota Makililo na Victoris Massawe wameendelea kuhamasisha wadau kuendelea kuchangia ujenzi huo. 

“Tunaomba wadau na Wizara ya Elimu kuona huruma kwa shule ya wasichana watusaidie kwenye kujenge uzio.Pia kwa unyenyekevu mkubwa tunamuomba Rais Samia Suluhu Hassan atusaidie kufanikisha ujenzi huu.Watoto kike wakihitaji kuangaliwa na amekuwa akilisemea hilo mara kwa mara,”ameongeza. 

Wakati huo huo Dada Mkuu wa Shule ya Sekondari Ruvu Jacquline Mgisha anayesoma kidato cha Sita alisema wanashukuru wanafunzi waliopita shuleni hapo kutambua umuhimu wa jambo hilo. 

“Uzio ni muhimu sana kwetu , hivi makazi ya watu yamekuwa karibu na shule na hivyo kuhatarisha usalama wa wanafunzi.Pia tunamuomba mama yetu Rais Samia Samia Suluhu kutusaidia na hatimaye tuwe na uzio na sisi tutamlipa kwa kufanya vizuri kwenye masomo,”amesema. 

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: