Moses Mashalla, Arusha 

HALMASHAURI ya jiji la Arusha imepokea kiasi cha sh,bilioni 2  kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 100 vya madarasa katika shule za  sekondari za jiji hilo ili ifikapo januari 2023  wanafunzi wote watakaochaguliwa kuingia kidato cha kwanza wawe wamejiunga na shule za sekondari. 

Mkuu wa wilaya ya Arusha,Said Mtanda amesema hayo leo wakati akiongea na wakuu wa shule za serikali jijini hapa na kutoa siku 75 kuanzia leo , ujenzi wa madarasa hayo uwe umekamilika kwa kiwango na ubora unaotakiwa.

Hata hivyo Mtanda alitahadharisha matumizi mabaya ya fedha hizo na kuwaonya wakuu wa shule watakaoenda kinyume na maelekezo ya serikali,kwamba watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Mtanda alisema  kwamba fedha hizo zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni mpango wa serikali wa kuhakikisha kila mwanafunzi anayefaulu elimu ya msingi anakwenda sekondari. 

"Rais aliahidi kuleta fedha za ujenzi wa madarasa na ametekeleza na tayari fedha hizo zipo kwenye akaunti yetu ya halmashauri  ya jiji la Arusha sh,bilioni 2"

Alizitaja shule  20 za sekondari zitazonufaika na fedha hizo ambazo tayari zimeshaingizwa kwenye akaunti zake kwenye mabano ni idadi ya madarasa ni pamoja na shule ya Arusha Day  sh,milioni 100 madarasa(5).

Shule zingine ni Arusha sekondari ,sh,milioni 160(8)Arusha Terat sh,milioni 140(7),Eleray sec sh,160(8),Felix Mrema sh,milioni 40(2),Kaloleni sh,mil.100(5),Kimaseki sh,mil 60(3),Lemara sh,mil.40(2) na Mkonoo sh,mil.20(1).

Zingine ni Movaro Sec.sh,mil 40(2)Mrisho Gambo sh,mil.80(4)Muriet sh,mil 220(11),Naura sh,mil 100(5),Ngarenaro mil. 100(5),Olasiti sh,mil 100(5),Olmoth sh,mil 60 na Olorien sh,mil.20(1).

Alitaja shule zingine kuwa ni Sinon sh,mil.280(14),Sombetini sh,mil 80(4) na Ungalimited sh,mil.100(5).

Mkuu huyo wa wilaya alionya vikali kwa wakuu washule watakaochelewesha mradi huo ama kwenda kinyume na matumizi ya fedha hizo ,
 kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufukuzwa kazi na  kifungo jela .

"Natoa wiki moja kwa kila shule iwe imeunda kamati zake za ujenzi na lazima wakuu wa shule wawashirikishe wazazi na kamati ya shule wawaeleze uwepo wa fedha hizo"

Alisema matumizi ya fedha hizo lazima yafuate mfumo wa serikali wa 'force account'kwa kila darasa lijengwe kwa sh,milioni 20 .

Awali mkurugenzi wa jiji la Arusha Hargeney Chitukulo alisema kuwa halmashauri  hiyo imepokea kiasi cha sh,bilioni 2 siku tatu zilizopita na tayari zimeingizwa kwenye akaunti za shule.

Chitukulo alisema atahakikisha madarasa yatakayojengwa yanakuwa na ubora unaohitajika na tayari ameteua msimamizi wa mradi katika kila shule zote  zinazonufaika na mradi kwa ajili ya kusimamia mradi huo.

"Tutahakikisha katika jiji la Arusha hakuna mwanafunzi aliyefaulu asijiunge na elimu ya sekondari mpaka sasa hatuna uhaba wa vyumba vya madarasa"

Share To:

Post A Comment: