DENIS CHAMBI, TANGA.
Mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini Thimotheo Mzava ameitaka kamati inayosimamia ujenzi wa shule ya Sekondari Mgwashi pamoja na viongozi wote kushirikiana na kuongeza kasi ya ujenzi huo ambao umeonekana bado unasua sau licha ya kutakiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu kama livyoelekezwa na serikali.
Mzava ametoa maagizo hayo jumatano wakati akipofanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa jimboni humo ambayo ni pamoja na mradi wa maji uliofikia asilimia 95 ya utekelezaji , ujenzi wa daraja lenye thamani ya milioni 50 uliokamilika,ujenzi wa ofisi ya kijiji pamoja na shule hiyo yenye madarasa 8, ofisi na maabara ambao unatarajiwa kuanza kutumika mwaka 2023 Mara baada ya kukamilika.
"Tumepata taarifa kutoka kwa viongozi wa wilaya kuhusu ujenzi huu nimefika eneo la mradi taarifa zile ni za uongo hazina ukweli nikirudi tunakwenda kumalizana nao huko huko, lakini sisi wananchi tusiwe kikwazo cha mradi huu kukamilika nawaomba Viongozi wote mnaosimamia pamoja na kamati zenu ongezeni jitihada na kasi ya ujenzi wa maradi huu uweze kukamilika kwa wakati, vifaa vyote ambavyo vinapatikana kwenye mazingira haya vichukueni kwa bei inayotambulika na kukubalika tusipokamilisha Ile shule tutawatesa watoto wetu wa Mgwashi"
"Kata yetu ya Mgwashi ni miongoni mwa kata ambazo hazina shule ya zekondari tulipambana tukapewa fedha na sisi ni watu wa kwanza kupata mapema kuna maeneo tumeyaacha hayana Sekondari, lakini tangu nimeanza ubunge moja ya shule ambazo zimetusumbua kwenye ujenzi wake hii ni kwa sababu kuna watu hawakuwa tayari na kuna wengine wanadanganya viongozi sasa kazi imesimama na tunavutana wenyewe kwa wenyewe" Alisema Mzava.
"Natamani ile kazi ikamilike kwa wakati inapokuja miradi kama hii pamoja na kutupa huduma sisi tutumie hiyo fursa wakati mradi inatekelezwa hatutegemei vibarua wayoke mbali wakati ndani ya kata yetu wapo vijana tutumieni ule mradi kama njia ya kupata kipato halali" aliongeza
Aidha Mzava amemuagiza afisa mtendaji wa kata ya Kwekibomi kufwatilia matumizi ya fedha shilingi laki nane alizozitoa kwaajili ya kuweka Umeme kwenye zahanati ya kata hiyo miaka mitano iliyopita lakini mpaka sasa hazijulikani zilipo na matumizi yake.
"Suala la Umeme wa kwenye zahanati ya Kwekibomi limenishtua sana maana wale wanalikumbuka suala hili nilishamalizana na nyinyi na nilitoa laki nane mwenyekiti na diwani hawaijui mtendaji wa kata japo ni mgeni tunataka utusaidie fedha kujua zilikwama wapi kwa sababu tulishatoa Kama zimetumika kivingine tujue na tumekwamishwa na nini" aliongeza Mbunge huyo.
Awali akizungumza mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Korogwe vijijini ambaye pia ni diwani wa kata hiyo ya Mgwashi Sadick Kallaghe alisema kuwa kwa kushirikiana na mbunge pamoja na wananchi wa wanaishukuru serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwaajili ya kutekeleza miradi ilivyokuwa na changamoto kwa kipindi cha muda mrefu.
"Tunaishukjru Sana serikali kwa namna jinsi wanavyoendelea kutuletea fedha za miradi katika kata ya Mgwashi, wito wangu kwa wananchi tuendelee kuitunza miradi hii ahadi yetu ni kutaka kuja kuwaonyesha watu mfano wa miradi ya maendeleo katika kata yetu na namna ya kuongoza tunataka kufanya Jambo ambalo litakaa milele na wale ambao wanatukwamisha hawana nafasi kwenye hii kata tunataka shule imalizike januari watoto waingie darasani wasome" alisema Kallaghe.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kata ya Mgwashi wameendelea kuishukuru serikali kwa namna miradi ivyendelea kutekelezwa kwenye kata hiyo huku waiomba kupelekewa umeme kwenye zahanati wanayoitumia pamoja na baadhi ya maeneo wanayoishi.
Aidha wakina mama wamelalamikia suala la kutokupata kwa wakati mikopo inayotolewa na halmashauri hiyo ambapo licha ya kuomba kwa muda mrefu na kupewa elimu ya mikopo hiyo wameshindwa kupatiwa hatua ambayo mbunge wa Jimbo hilo ameichukuwa na kumtaka mwenyekiti wa halmashauri kufwatilia suala hilo na kulipatia ufumbuzi.
"Sisi wananchi wanawake tunayo shida ya kupata mikopo tumepatiwa elimu ya mikopo mara kwa mara na tumeomba muda mrefu lakini mpaka Sasa hatujapata tunaomba tusaidiwe kupatiwa mikopo"
"Tuna furaha kubwa sana kwaajili ya miradi mliyotuletea ikiwemo mradi wa shule , barabara na ujenzi wa ofisi, shida tuliyonayo ni Umeme katika zahanati yetu muda mwingine ukiwa una shida ya shindano za masaa tumekuwa tukitumia tochi " walisema wananchi hao.
Post A Comment: