Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akifurahia na wananchi wa kitongoji cha Ikanka katika kijiji cha Itumba wilayani Ileje mkoa wa Songwe wakati Kamati ya Mawaziri Nane inayoshughulikia migogoro ya Matumizi ya Ardhi katika vijiji 975 ilipotembelea kitongoji hicho
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akizungumza katika kikao na wananchi wa kitongoji cha Ikanka katika kijiji cha Itumba wilayani Ileje mkoa wa Songwe wakati Kamati ya Mawaziri Nane inayoshughulikia migogoro ya Matumizi ya Ardhi katika vijiji 975 ilipotembelea kitongoji hicho
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (wa pili kulia) na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula wakimsaidia Bi Eliminia Mbuhi mkazi wa kitongoji cha Ikanka katika kijiji cha Itumba wilayani Ileje mkoa wa Songwe wakati Kamati ya Mawaziri Nane inayoshughulikia migogoro ya Matumizi ya Ardhi katika vijiji 975 ilipotembelea kitongoji hicho
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ametaka wafugaji kumilikishwa ardhi na kupatiwa hati kwa ajili ya shughuli za ufugaji.
Naibu Waziri Ulega ametoa kauli hiyo Oktoba 24, 2022 mkoani Songwe kwa nyakati tofauti wakati Kamati ya Mawaziri nane wa Wizara za Kisekta inayoshughulikia migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 ilipozungumza na uongozi wa mkoa wa Songwe pamoja na kutembelea wananchi wa kitongoji cha Ikanka kijiji cha Itumba wilayani ileje.
Alisema, wakati ikisisitizwa ardhi inayomegwa kwenye maeneo mbalimbali ya hifadhi kupangiwa mipango ya matumizi ni wakati muafaka sasa kwa ardhi hiyo nayo kutolewa kwa shughuli za mifugo na wamiliki wake kupatiwa hati.
‘’ kwa nini tuna mashamba ya kilimo mazao mengi na kwa nini kilimo mifugo hakina hati? Wafugaji wana hamasa za kutaka kununua na kumiliki ardhi kwa kuwa siyo masikini na uwezo wanao’’ alisema Ulega
Aliongeza kwa kusema kuwa, hatua ya kuyapatia mashamba mifugo hati mbali na kuwasaidia wafugaji kuwa na umiliki wa ardhi lakini itawazuia kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine sambamba na kuwatambua kwa urahisi ambapo alisema kwa sasa inakuwa vigumu hata wafugaji kukopesheka wakati ni matajiti.
Alisema, haiwezekani kumaliza migogoro ya ardhi kwa maneno na watendaji katika ngazi zote wanapaswa kufanya kazi kwa vitendo na kusisitiza kuwa hata kama utekelezaji huo utaanza kwa mfugaji mmoja mmoja itasaidia na kutaka watendaji kubadilika ili kuiboresha sekta ya mifugo.
Kwa mujibu wa Ulega, pamoja na kuwepo fursa nyingi za uhitaji wa nyama kwenye nchi mbalimbali duniani na Tanzania kuwa na idadi kubwa ya mifugo kama vile ng’ombe, mbuzi na kondoo lakini imeshindwa kuchangamkia fursa hiyo.
Alisema kwa sasa wizara yake inaboresha sera ya mifugo na kutaka kila mmoja kushiriki katika kuhakikisha sekta ya mifugo inaimarika na kufanya vizuri.
Post A Comment: