Na Veronica Mheta, Arumeru
Mfanyabiashara maarufu wilayani Arumeru Mkoani Arusha,Itandumi Makere atazikwa jumamosi Machame Mkoani Kilimanjaro.
Makere ambaye alikuwa ni mmiliki wa jengo la Rotterdam lililopo karibu na kituo cha Polisi Usa-river ametoa ajira kwa watu mbalimbali ikiwemo kujitoa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) pamoja na serikali.
Kifuatia msiba huo , Katibu Mwenezi Wilaya ya Meru, Kennedy Mpumilwa amewaongoza baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM Wilaya ya Meru kutoa pole nyumbani kwa mfanyabiashara huyo eneo la USA -River wilayani Arumeru.
Mfanyabiashara alifikwa na mauti juzi na anatarajia kuagwa kesho na kwenda kuzikwa kwao Machame Mkoani Kilimanjaro.
Akitoa pole nyumbani kwa mfanyabiashara huyo, Kennedy amesema marehemu alikuwa ni mfanyabiashara na mtu aliyejitoa kwa watu ikiwemo kutoa ajira mbalimbali kwa vijana na jamii kwa ujumla.
Amesema chama kimepata pigo kutokana na msiba huo hivyo alitoa pole kwa familia na jamii kwa ujumla kutokana na kifo cha mfanyabiashara Makere.
Wakati huo huo, Mpumilwa amemtembelea diwani wa kata ya USA-river,Omary Mshana aliyetenguka mguu kwaajili ya kumpa pole
Post A Comment: