BARAZA la madiwani Manispaa ya Mtwara Mikindani, limepitisha rasimu ya sheria ndogo, ili kupelekwa kwa Waziri mwenye dhamana azipitishe na kuanza kutumika katika halmashauri hiyo.
Sheria hizo ni pamoja na sheria ndogo za uanzishwaji wa mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa, sheria ndogo za afya na usafi wa mazingira , sheria za kilimo na usalama wa chakula.
Sheria nyingine ni sheria ndogo za ujenzi mjini, za ada na ushuru, usimamizi wa masoko pamoja na sheria ndogo za mji Mkongwe wa Mikindani.
Mchakato utungaji Sheria ndogo hizo ulianza Januari mwaka huu kwa kukusanya maoni na mapendekezo kutoka kwa wananchi pamoja na wadau wengine wa maendeleo.
Post A Comment: