Na John Walter-Manyara
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brand Ltd David Mulokozi ametoa msaada wa Fimbo nyeupe 500 kwa watu wasioona ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kusaidia makundi yenye mahitaji maalum.
Akikabidhi fimbo hizo kwa mgeni rasmi Patrobas Paschal Katambi Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) aliyemwakilisha waziri mkuu Kassim Majaliwa, Mulokozi amesema kampuni hiyo itaendelea kuiunga mkono serikali kwa kila jambo ili kupunguza changamoto kwa Wenye ulemavu
Katambi amemshukuru Mulokozi kwa msaada huo na kumpongeza kwa moyo wa upendo akiita kitendo hicho ni ibada kubwa na linapaswa kuigwa na wengine.
Madhimisho ya fimbo nyeupe duniani, nchini Tanzania kitaifa yamefanyika katika mkoa wa Manyara mjini Babati na kuhitimishwa leo oktoba 21,2022.
Kaulimb mbiu ya Fimbo Nyeupe mwaka huu inasema “Watu wasioona,tujumuishwe katika ajira,michezo na Teknolojia ya habari na mawasiliano kwa maendeleo endelevu”.
Post A Comment: