Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake namna ambavyo serikali kuu imetoa kiasi cha shilingi milioni 900 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule za sekondari 
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake namna ambavyo serikali kuu imetoa kiasi cha shilingi milioni 900 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule za sekondari.


Na Fredy Mgunda,Iringa.

 

HALMASHAURI ya Manispaa ya Iringa imepokea pesa kiasi cha Milioni 900 kutoka serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 45 ya shule za sekondari.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada alisema kuwa Manispaa ya Iringa ilikuwa na uhitaji wa madarasa 56 ambayo yanatakiwa kujengwa katika shule za sekondari.

Ngwada alisema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoka pesa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 45 hivyo wameisaidia Manispaa katika ujenzi wa madarasa hayo.

Alisema kuwa madarasa 11 yaliyobaki yatajengwa kwa kutumia mapato ya ndani kwa sababu serikali kuu imewapunguzia mzigo wa ujenzi wa madarasa hayo.

Ngwada alisema kuwa kiasi hicho cha pesa za ujenzi wa madarasa 45 itahusika katika shule kumi na nne (14) zilizopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.

Alisema kuwa shule hizo kumi na nne (14) ni shule ya Sekondari Ipogolo madarasa 5,Kigungawe madarasa 3,Kihesa madarasa 4,Kleluu mazoezi madarasa 4,Kwakilosa Darasa 1,Lugalo darasa 1,Mawelewele madarasa 4,Mivinjeni Idunda madarasa 3,Mlamke Darasa 1,mlandege madarasa 4, Mtwivila madarasa 5,Shabaha madarasa 3,Nduli madarasa 4 na Tagamenda madarasa 3 ambapo kila darasa litaghalimu kiasi cha shilingi million ishilini (20,000,000)

Meya Ngwada alisema kuwa pesa hizo zitaingia moja kwa moja kwenye akaunti za shule husika hivyo walimu na viongozi watakuwa wanazisimamia wanatakiwa kuwa makini na fedha hizo kwa ajili ya kuleta matokeo chanya yanayokusudiwa.

Ngwada alimazia kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo za ujenzi katika kukuza sekta ya elimu na kuwaondolea usumbufu wazazi wa kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa 45.

Aliwaomba wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kumuunga mkono Rais kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo kwa wananchi wa Tanzania kwa ujumla wake.

Share To:

Post A Comment: