DENIS CHAMBI , TAGA.
Michuano ya kusaka vipaji vya mchezo wa ngumi inayoendelea kata kwa kata ndani ya jiji la Tanga maarufu kama Five brothers boxing championship msimu wa pili inaendelea kuteka mashabiki na wadua wa mchezo huo kwenye viwanja mbalimbali wakishuhudiwa mabondia wengi wakionyeshana ubabe kupitia ngumi za ridhaa.
Mashindano hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya five brothers entertainment yamelenga kuongeza hamasa ya mchezo huo wa ngumi ndani ya jamii pamoja na kutoa fursa kwa mabondia chipukizi wenye ndoto za kuja kupanda ulingoni na kucheza ngumi za kulipwa wakitarajia kuiheshimisha Tanga kwa kupambania mikanda mbalimbali ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Akizungumza muandaaji wa mashindano hayo na mkurugenzi wa kampuni ya five brothers entertainment Nassoro Makau 'Nassa' alisema kuwa "ujio wa mashindano hayo ya kata kwa kata hasa yana lengo la kutoa kuongeza hamasa ya mchezo wa ngumi Kwenye jamii na kutoa fursa kwa mabondia wachanga wenye ndoto za kupanda ulingoni na kupambania mikanda mbali mbali ili wapate nafasi ya kuonyesha walicho nacho kwenye mchezo huo ili waweze kutimiza ndoto zao kupitia "
Nasa ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha ngumi ya ridhaa wilaya ya Tanga 'AMACHA' amesema wamedhimia kufikia malengo yao walio jiwekea na kufufua matumaini yaliyopo ndani ya mchezo wa masumbwi hasa kwa rika la vijana ambao wameonekana kuvutiwa na uwepo wa mabondia kama Hassan Mwakinyo , Salimu Mtango na wengineo wanaoiwakilisha vyema Tanga na Tanzania kwa ujumla wamekuwa ni chachua kwao kuipenda mchezo huo.
Wiki ijayo itakuwa ni bandika bandua tena kwani jumanne ijayo ngumi zitaendelea kwenye viwanja vya Msambweni wakati kesho yake itakuwa ni zamu ya wanamasumbwi kutoka kata ya Duga huku alhamisi ngumi hizo zikitarajiwa kuchapwa kata ya Maweni kwenye uwanja wa Magereza.
Post A Comment: