Meneja wa NSSF Mkoa wa Tanga Audrey Claudius  kushoto akimkabidhi  cheti na tuzo Mkuu wa Idara ya Fedha ya Tanga Cement Isaack Mponela kwa kuibuka washindi wa jumla katika mwajiri mkubwa anayechangia mchango  ndani ya mfuko huo 




Na Oscar Assenga,TANGA.

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF)mkoa wa Tanga mwishoni mwa wiki wamehitimisha wiki ya huduma kwa wateja huku wakitambua umuhimu wa waajiri hususani wakubwa kwa kuwapatia vyeti na vikombe ikiwa ni kuthamini mchango wao kwa kuchangia wazuri katikia mfuko huo

Akizungumza mara baada ya zoezi hilo Meneja wa NSSF Mkoa wa Tanga Audrey Claudius alisema kwamba katika wiki hiyo ambapo alisema waliwapa vyeti ambavyo zinaonyesha mchango wao kama waajiri wakubwa na waliwaweka kwenye makundi mbalimbali kwenye waajiri wakubwa na
wanaolipa michango kwa wakati na wenye taarifa nzuri nzuri.

Aidha alisema kwamba waajiri hao wamekuwa na mchango mkubwa ndani ya mfuko huo huku akihaidi kushirikiana nao kuhakikisha wanaendelea kupata mafanikio.

"Niwapongeze waajiri tuendelee kufanya vizuri kwa vipindi vyenginevyo vyote kwani kwa kufanya vizuri kunachangia nasi kuweza kutoa huduma nzuri na kwa wakati hivyo ni muhimu kushirikiana" Alisema Meneja huyo

Aidha alisema katika kipindi cha wiki ya huduma kwa mteja kwa mkoa huo wanachama walio wafungulia madai zaidi ya 15 na yote yamefanikiwa kulipwa na hiyo inatokana na waajiri kuwajibika ipasavyo kwa kupeleka michango yao kwa wakati na taarifa za wanachama kiwa sahihi.

"Niwasihi wafanyakazi wenzangu tuendelee niwashii wafanyakazi wenzangu tuendelee kushirikiana kuweza kufanya vizuri zaidi lakini Tanga Cement ni mwajiri mkubwa anayechangia mchango mkubwa kwa Mkoa wa Tanga na ndio mshindi kwa ujumla”Alisema

Naye kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Fedha ya Tanga Cement Isaack Mponela kwa niaba ya waajiri wote aliwashukuru ofisi ya Mfuko huo mkoani Tanga kwa kushirikiana pamoja nao katika wiki ya huduma kwa mteja..

Mponela alisema katika wiki ya huduma kwa mteja na ile huduma nzuri kwa wateja wao kama waajiri na nmwanachama wa mfuko Mfuko huo wanaipata siku zote.

Alisema kwamba mfuko huo unafanya vizuri kuhakikisha mahusiano kati yao na wanachama wakiwemo waajiri yanakuwa mzuri sana.

Alisema wao kama Kampuni wanatoa kipaumbele pamoja na kufuatilia na kushika sheria za nchi ikiwemo ya Mfuko huo hivyo ni jukumu lao kuhakikisha michango inafika NSSF na waajiri wote wanajiunga na mfuko huo kwani wao wanatoa kipaumbele kuhakikisha taratibu za nchi
zinafuatwa.

Naye kwa upande wake Mwanachama wa Mfuko huo Mkoani Tanga,Ally Juma alisema kwamba wanashukuru walifungua madai na amelipwa kwa wakati huku akiwataka watanzania kuendelea kujiunga na Mfuko huo iki kuweza kuendelea kunufaika na huduma mbalimbali.

Mwisho.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: