Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mhe Chief Mwita Waitara ametoa msimamo wake Rasmi kuhusu usimamizi wa fedha zinazotolewa na Mgodi wa North Mara uliopo Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara ikiwa ni wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM wilaya Tarime Mapema leo
Mbunge Waitara amesisitiza kuwa amejipanga kuhakikisha fedha hizo za uwajibikaji CSR zinasimamiwa Ipasavyo kwa lengo la kutekeleza Miradi ya Maendeleo itakayowanufaisha Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya Tarime
Aidha Mhe Waitara amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu fedha hizo za Uwajibikaji (CSR) kuanza kutumika
Mbunge Waitara pia amwongeza kuwa wao kama Halmashauri ya Wilaya Tarime chini ya Mwenyekiti Simon Kiles wamekubaliana kufanya mgawanyo wa fedha hizo Ili ziweze kuwanufaisha Wananchi wa Halmashauri nzima tofauti na ilivyokuwa Hapo Awali zilikuwa zikipelekwa kwenye Vijiji 11 pekee vinavyozunguka Mgodi huo vilivyomo ndani ya kata tano
Hivyo mgawanyo wa fedha hizo itakuwa 70% zitapelekwa kwenye Vijiji 11 vinavyozunguka Mgodi huo huku 30% zikipelekwa katika Vijiji vingine kwa lengo la kuhakikisha fedha hizo zinakuwa na faida Kwa Wananchi wote wa Halmashauri ya Wilaya Tarime
" Kulikuwa na wizi mkubwa kwenye fedha hizi za CSR na tulikuwa hatuna uongozi ambao ni Makini katika kusimamia ,Niwahakikishie Wananchi wa jimbo langu la Tarime Vijijini kuwa fedha hizo tutazisimamia Ipasavyo kwa lengo la kuleta Maendeleo" Mhe Chief Mwita Waitara Mbunge wa jimbo La Tarime Vijijini akizungumza na waandishi wa habari
Post A Comment: