MAHAKAMA ya Hakimu mkazi Kisutu imempa siku 14 aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda meiahirisha kesi ya madai inayomkabili aliyekuwa Mkuu kuwasilisha utetezi wake mahakamani hapo dhidi ya kesi ya madai ya gari inayomkabili yeye pamoja na William Malecela, almaarufu kama Le Mutuz.


Hatua hiyo imekuja kufuatia wakili wa anayemuwakilisha Makonda, Gift Joshua kudai mahakamani hapo kuwa mteja hajapelekewa hati ya madai.

Kesi hiyo ya madai namba 234/2022 ambayo leo Oktoba 13, 2022 imetajwa kwa mara ya kwanza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Richard Kabate, imefunguliwa na Patrick Kamwelwe mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.

Mapema wakili wa mdai, Consolata Mtana alidai mahakamani hapo kuwa kesi leo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba walishampatia mdaiwa namba moja (Lemutuz)hati ya madai lakini walishindwa kumpata mdaiwa namba mbili (Makonda) kwa kuwa wamemtafuta bila ya mafanikio.

Hata hivyo wakili anayemuwalilisha Makonda, Gift Joshua baada ya kukabidhiwa hati ya madai aliiomba mahakama kumpatia siku 14 ili aweze kufaili utetezi wake.

Katika hati yake madai yake, Kamwelwe anadai yeye alikuwa anamiliki gari aina ya Range lover ambapo kutokana na urafiki wake na Lemutuz na urafiki kati ya Lemutuz na Makonda ndio Makonda aliomba kuitumia ile gari .

Anadai Yeye alimkabidhi Lemutuz gari hiyo ili ampatie Makonda aweze kuitumia wakati alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kwamba katika makubaliano yao ilikuwa ni kwamba angeitumia gari hiyo kwa kipindi cha wiki mbili kisha angeirudisha lakini haikuwa kama waliyokuwa wamekubaliana, baada ya wiki mbili kukamilika bado Makonda aliendelea kuitumia hiyo gari na mpaka leo hajarejeshewa gari yake.

Pamoja na mambo mengine mdai anaiomba mahakama kurejeshewa thamani halisi ya kiasi cha pesa alichotumia kununulia hiyo gari, anadai pesa ya usumbufu, garama za kutokuwa na gari yake kwa kipindi chote hicho.

Pia, Kamwelwe anaiomba mahakama imuamuru Makonda na mwenzake, kumlipa kiasi hicho cha fedha kama fidia anayodai kuwa, imetokana na hatua ya wadaiwa hao kumdhulumu gari lake jeusi aina ya Toyota Rand Rover/Range Rover Ronge Sport, yenye namba 20153.

Katika mchanganuo wa fedha hizo, Sh. 247,243,750, ambazo ni sawa na dola za Marekani 106,250, Kamwelwe anamtaka Makonda na mwenzake, walimpe dola 11,250, kama gharama ya kodi ya kuliingiza gari hilo. Dola 50,000, fidia ya kutwaa gari, pamoja na dola 45,000, ambayo ni thamani ya gari.

Kesi hiyo itatajwa tena Novemba 8, 2022

Share To:

Post A Comment: