MAFUNDI zaidi ya 1000 nchini, watapatiwa elimu kuhusu masuala ya upauaji wa nyumba.
Hayo yamesemwa leo na Meneja wa Kampuni ya ALAF, Mikoa ya Kanda ya Ziwa, Adam Nelson, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mtu Kwao.
Nelson amesema kupitia kampeni hiyo, wanatarajia kuwafikia mafundi zaidi ya 1000 kutoka mikoa yote ya kanda ya Ziwa.
‘’Katika kampeni ya Mtu Kwao, itasaidia sana kwa mafundi wa ujenzi kubadilishana uzoefu katika tasnia ya uwezekaji nyumba.
“Pia mafundi katika kampeni hii watapata ujuzi mbalimbali kwa teknolojia za kisasa,’’ amesema Nelson.
Amesema kampeni hiyo itasaidia kuhamasisha Watanzania kuweza kununua bidhaa mbalimbali za ujenzi kutoka kampuni yao.
Amesema kupitia mafunzo yao, wanaomba mafundi waweze kufanya kazi za kisasa zaidi, waweze kujenga majengo bora ya kisasa.
Post A Comment: