Kiteto-Manyara

Makundi maalumu ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu wanakusudiwa kunufaika na mkopo wa asilimia 10% sawa na mil 200 ambayo ni mapato ya ndani ya Halmashauri ya Kiteto Mkoani Manyara kwa mwaka 2022-2023.

Wanufaika wa kiasi hicho cha fedha ni vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, ambao Serikali imeweka mpango wa kila mwaka halmashauri kutenga Asilimia 10% ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya makundi hayo.

“Hili ni Takwa la kisheria ambalo Halmashauri inatakiwa kutenga kiasi cha asilimia 10% ya mapato yake ya ndani na kugawa kwa makundi hayo ambapo vijana wamepangiwa 4%, wanawake 4% na watu wenye ulemavu 2%.” Alisema John Nchimbi Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kiteto.

Alisema kiasi hicho kinachokopeshwa na halmashauri kwa makundi hayo hakina riba kwenye marejesho, lengo la Serikali ni kuinua kipato cha makundi hayo ambayo kwa siku za hivi nkaribuni yalionekana kuwa duni kimaisha huku vijana wakitegemewa kuwa nguzo kuu ya Taifa

Nchimbi alisema kwa mwaka 2021-2022 Halmashauri ilitoa asilimia 18% ya mapato yake ya ndani sawa na kiasi cha mil 180 ambacho kiliwezesha vijana kiuchumi hivyo kwa mwaka 2022-2023 halmashauri ya Kiteto wanakusudia kuongeza kiasi hicho hadi kufikia mil 200.

Kuhusu marejesho Nchimbi alisema halmashauri imejipanga kuhakikisha kuwa mikopo hiyo inarejeshwa kwa wakati kwani wanakopesha mtu mwenye namba za Nida na kuingizwa kwenye mfumbo ambao kama hatorejesha hawezi kukopesheka popote nchini.

Nao baadhi ya vijana akiwemo Mohamed Issa (Kibaya) alisema mikopo inayotolewa na halmahauri haina usumbufu tofauti na taasisi zingine za Kibenki kwani wamekuwa wakiuzia vitu vyao vya ndani mpaka hata lengo la kuongeza kipato linatoweka.

“Mimi niliwahi kukopa sehemu hakika nilichelewa kurejesha nilipigwa riba lakini ilifika mahali nilikamatiwa kochi vitanda na vitu kadha vya ndani ya nyumba jambo ambalo liliondoa hata maana halisi ya mkopo kwa maana ya kuongeza kipato”alisema Issa.
Share To:

Post A Comment: