Na. DENIS CHAMBI, TANGA.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo ameunda kamati ya watu 11 kuchukungaza kwa kina sababu zilizopelekea kuungua Moto ghala lililokuwa limehifadhia bidhaa za magendo katika Bandari ya  TANGA  zilizoingizwa kwa njia ya zilisizo rasmi ambapo zote ziliteketea.

Tukio hilo  lilitokea saa nane na nusu za usiku wa kuamikia  October 23 ambapo kulikuwa na beri za vitenge, mafuta ya kula  , sukari , pikipiki zilizokamatwa zikibeba bidhaa za magendo baiskel, injini nne za boti, galoni za Diesel na bidhaa  nyinginezo vyote vikiwa na thamani ya shilingi Million 541, 729, 519.35 ambapo  Kodi yake jumla iliwa ni million 423, 6,872. 04.

Akizungumza na vyombo vya habari Mgumba ofisini kwake   amesema kuwa kamati hiyo ambayo itajumuisha mtaalamu kutoka Tanesco, zimamoto na uokoaji , ofisi ya Rais,  jeshi la Polisi, taasisi ya kuzuia na kupambana na rusha "TAKUKURU"  TBA, ofisi ya mkemia mkuu , mwanasheria mkuu  wahandisi  pamoja na ofisi ya mkuu wa mkoa itatakiwa kufanyia kazi  uchunguzi huo ndani ya siku saba Kisha kupeleka majibu ya kile ambacho wamekibaini.

"Mpaka sasa tunachukulia ni ajali ya noto kama zilivyo ajali nyingine lakini tunataka tujiridhishe twende mbali zaidi ndio maana tumeamua kuunda timu maalumu kwaajili ya kuchunguza tukio hilo ili kijiridhisha sababu na chanzo chake nini" alisema Mgumba.

"Tulichokifanya baada ya kupata taarifa tulizima moto na tumefanikiwa japo hatukuokoa chochote kilichokuwa ndani ya ghala  lakini tuliitisha kikao na kamati  ya ulinzi na usalama  ya mkoa lakini pia tumeunda kamati maalumu ya watu 11ambayo itafanya kazi hii ya uchunguzi ndani ya siku saba"

Mgumba alisema moja wapo ya vitu vitakavyochunguzwa ni kuchelewa kwa taarifa  kutoka Mamalaka ya mapato Tanzania akiwemo mmoja wa Watumishi wa Mamalaka hiyo na kikosi cha kuzuia magendo  cha mkoa ambapo mara baada ya kutokea kwa tukio hilo alitafutwa kwa njia ya Simu lakini hakupokea mpaka kamati ya ulinzi na usalama ilivyofika katika eneo hilo.

"Kamati hii mara baada ya kuchunguza tunatarajia watuambue chanzo ni nini kama kuna hitilafu ya umeme au hujuma iliyofanyika lakini kupitia nyaraka zote za mamalaka ya mapato kuhusu mizigo na kuhakiki mali zilizopo,kuchunguza muda wa taarifa miongoni mwa vitu tulivyoona ni kwamba taarifa zilichelewa kuna mmoja wa mtumishi wa TRA ambaye yupo kwenye timu task force ya mkoa ya kikosi cha kuzuia  magendo  alipofiwa Simu tangu tukio lilivyotokea mpaka asubuhi alimpigiwa Simu lakini hakupokea kwahiyo lazima achunguzwe" aliongeza Mgumba.

Aidha alisema mara baada ya kamati hiyo kuundwa serikali inaendelea kuwahakikishia ulinzi na usalama amewatoa hofu wananchi na watanzania kwa ujumla kuwa hali ya Usalama iko shwari  ikizidi kusimamiwa na vyombo vyote vya ulinzi na usalama  ikiwa ni pamoja na kuimarisha doria za mara kwa mara  huku akiwataka kuendelea na shughuli zao za kulijenga taifa na kulipatia kipato.

"Baada ya hiyo kamati serikali tulichoamua ni kuendelea kuwahakikishia wananchi wa mkoa wa Tanga na Tanzania kwa ujumla kumba hali ya usalama kwa mkoa wa Tanga iko shwari na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama viko makini na vinaendelea kila taarifa ambayo tunaweza kuipata, nimevitaka vyombo vyote vya ulinzi na usalama kuhakikisha ulinzi na usalama hususani katika kuimarisha doria ikiwemo  kwenye taasisi zetu za  fedha na kwenye miundombinu mikubwa ya viwanda na biashara pamoja na sehemu zinazokusanya watu wengi zaidi kama viwanda doria ziwepo za mara kwa mara" aliendelea.

Hata hivyo Mgumba licha ya kuunda kamati hiyo maalumu amevitaka vyombo vyote vya ulinzi na usalama kuanza uchunguzi kwa upande wao ndani ya siku saba na hatimaye kupeleka majibu  ya tukio hilo ambalo limeteketeza zaidi ya shilingi Million 950 katika ghala hilo liliokuwa  katika Mamalaka ya Bandari Tanga.

"Pamoja na kuunda kikosi kazi hichi au timu maalumu ya wataalamu  bado nimevitaka  vyombo vyote vya ulinzi na usalama  katika mkoa wa Tanga vya kiuchunguzi kuanza uchunguzi wa tukio lile kuanzia leo (Jana jumapili) wao wasisubiri taarifa ya kiuchunguzi wa timu tuliyoiunda  wao wanaanza uchunguzi Leo na waniletee taarifa ndani ya siku saba hizo hizo ili taarifa iwe imekamilika kwa sababu ni jukumu lao la msingi" 

Mgumba aliwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ikiwemo wanaofanya biashara kinyume cha taratibu na sheria za nchi  ikiwemo  biashara za magendo ili kuvikomesha vitendo hivyo ambavyo kwa namna moja ama nyingine vinachangia kudumaa  na kurudisha nyuma maendeleo ya kukua kwa  uchumi wa taifa na wananchi kwa ujumla.

" Niendelee kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano wanaoutoa  wa kutupa taarifa  kuhusu Vita hii vya kupambana na magendo lakini nitoe wito  kwa wananchi kuendelea kufanya biashara halali kwa mujibu wa sheria kwa sababu biashara ya magendo siku zote ni patapotea , wananchi nyumba zao zisitumike kuhifadhia biashara za magendo kuhifadhia waharifu au wahamiaji haramu wa aina yeyote ile kwa sababu kufanya hivyo ni kuiangamiza  nchi yako"

Mgumba alisema kuwa serikali  ndani ya mkoa wa Tanga katika kupambana na wahalifu, uhalifu na biashara haramu  imeendelea kurasimisha Bandari bubu zote zilizokuwa zikitumiwa kama mianya ya kupitisha magendo, kupeleka Watumishi wa Umma katika mipaka yate iliyopo , kuimarisha doria za majini na nchi kavu kwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, kuimarisha  fukwe  ili kuwapa wawekezaji mbalimbali kuzimiliki ziwe ni chanzo cha mapato kwa taifa .


Share To:

Post A Comment: