Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro leo Tarehe 18/10/2022 ameanza ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa 29 ambavyo vitagharimu kiasi cha shilingi milioni 580

Mhe. Muro ambae ametembelea sekondari za ikungi, unyahati, puma pamoja na dadu amesema kazi imeanza katika shule za sekondari 16 ambapo amesisitiza madarasa kujengwa kwa viwango vyenye ubora wa thamani halisi ya fedha 

Dc Muro amemshukuru Mheshimiwa Rais. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia wilaya kupata milioni 580 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa ya shule 16 za sekondari

Dc Muro amesema fedha zilizotolewa zinatosheleza kujenga vyumba vipya vya madarasa 29 ambayo yatamaliza uhaba wa vyumba kwa wanafunzi wapya wanaotarajiwa kupokelewa katika msimu mpya wa masomo January 2023 

Tayari Mkurugenzi wa halmashauri Mhe. Justice Lawrance ameshazielekeza fedha hizo katika akaunti za shule ambazo zitateleleza miradi hiyo ili kurahisisha mchakato wa ujenzi na kuweka uwazi katika matumizi ya fedha husika 



Share To:

Post A Comment: