DENIS CHAMBI, TANGA
Halmashauri ya jiji la Tanga imejipanga kurudisha historia yake ya viwanda kama ilivyokuwa zamani hatua ambayo itakwenda kuchangia maendelo kwa wananchi na kuongeza pato la Taifa ambapo imetenga jumla ya hekta 3134 kwajili ya ujenzi wa viwanda mbalimbali .
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri jiji hilo Dkt Sipora Liana wakati akizumgumza na waandishi wa habari ofisini kwake kutangaza juu ya fursa na maeneo ya uwekezaji yaliyopo ndani ya jiji la Tanga ambapo amesema kuwa maeneo yote yaliyotengwa ni rafiki kwaajili ya uwekezaji akitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
"Wengi wa wakazi wa jiji la Tanga wanajishughulisha na kilimo lakini baada kilimo kile watu wanakuwa hawana kaz kwahiyo tunakaribisha wawekezaji waje kwaajili ya shughuli za viwandani, viwanda ni muhimu sana kwaajili maendeleo ya uchumi , tuna maeneo ya viwanda katika sekta ya madini zaidi ya hekta 212, tuna hekta 3134 kwaajili ya uwekezaji wa wakuzalisha bidhaa mbalimbali na maeneo haya yameshapimwa" alisema
"Jiji la tanga katika miaka ya nyuma wakati ilipokuwa ni manispaa lilikuwa na viwanda vingi sana lakini vile viwanda ukiangalia kwa sasa hivi vingi vimesimama havina uzalishaji kwahiyo tunataka tufanye amsha amsha kwaajili ya Tanga hasa kwaajili ya kuleta mabadiliko ya kiuchumi ya jiji la Tanga na nchi kwa ujumla". alisema Dkt. Liana
"Pia kuinua uchumi wa wananchi na hapa tutagusa hasa uchumi wa wananchi wa chini ambao ni asilimia 75 hadi 80, na ukiangalia jiji la tanga limebarikiwa ardhi yake yenye rutuba inafaa kwa sekta ya kilimo kwa mazao mbalimbali kuna matunda mengi sana yanayotoka katika jiji la Tanga ambayo yanapelekwa ndani na nje ya nchi yetu na maeneo tunayo kwahiyo tunawalika wawekezaji waje kuwekeza"
Hata hivyo mkurugenzi huyo ameongeza kuwa wapo baadhi ya wawekezaji wameshaonyesha nia ya kuja kuwekeza ndani ya jiji la Tanga na kuwa maeneo yote yaliyotengwa yana huduma mbalimbali za kijamii huku jiji hilo likiendelea kufikisha huduma zile muhimu zikiwemo maji umeme barabara pamoja na vituo va afya.
"Haya maeneo yote yana miundombinu mfano kwa upande wa maji mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira "Tanga uwasa" wanaendelea kupanua na kuongeza wingi wa maji na wanajua huko mbeleni kutakuwa na watu wengi na wapo baadhi ya wawekezaji tayari wamewshaanza kuonyesha nia ya kuwekeza tangu mwezi wa 7.
Aidha Dkt. Liana amewatoa hofu wawekezaji kuwa hakutakuwa na urasimu wowote wa kupata vibali vya maeneo ambayo tayari yameshapimwa na kuahidi kutoa ushirikianio kwao katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa kila mmoja.
"Sasa hivi uzalishaji ni mdogo sana utakuta wazalishaji ni wadogo wadogo wanazalisha kama tani elfu 6 hizi hazitoshi kwahiyo tunawakaribisha wawekezaji wakubwa na wadogo na tunaahidi kuwa hakutakuwa na urasimu mazingira tutayaweka ya muda mfupi ya wao kupata maeneo kwa muda mfupi sana " aliongeza.
Hata hivyo ameongeza wanatanguliza masahi ya taifa wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi sambamba na kukaa pamoja na wawekezaji kuweza kufuata sheria na taratibu za nchi katika uwekezaji.
Jiji la Tanga lina ukubwa kilometa za mraba 600 ikijumuisha sehemu ya eneo la bahari lenye kilometa za mraba 62 .
Post A Comment: