Halmashauri ya Mji wa Mbinga yapokea Jumla ya Tsh 220 milioni kwaajili ya Ujenzi wa Madarasa katika shule za Sekondari 7.  ya mapokezi ya fedha hizo kamati ya fedha na mipango   Halmashuri ya Mji wa Mbinga, imefanya ziara katika shule hizo na kutoa maelekezo juu ya utekelezaji wa miradi hiyo ambapo baadhi ya shule  hatua za awali za utekelezaji wa miradi hiyo zimeanza.


Kamati hiyo ya fedha ambayo ilijumuisha pia wataalamu wa Halmashauri ilisisitiza swala la ushirikishwaji wa wananchi katika utekelezaji wa miradi hiyo na kuzitaka kamati zilizoundwa ngazi ya shule kushirikiana na uongozi wa Kata ili kuweza kumaliza miradi hiyo kwa wakati.



Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Mbinga Bi Grace Quintine aliwataka  walimu wakuu kujenga utamaduni wa kubana matumizi (saving) ili kuhakikisha fedha hizo zinakamilisha miradi, sambamba na upatikanaji wa madawati katika vyumba hivyo vya madarasa.


Hata hivyo Bi Grace alizikumbusha Kamati kutunza nyaraka zote muhimu katika faili la mradi, pamoja na kuandaliwa kwa kitabu cha mradi kwa ajili ya maelekezo pindi viongozi watakapo tembelea kawaajili ya ukaguzi wa miradi hiyo.

Share To:

Post A Comment: